Header Ads Widget

SOUWASA SONGEA YAPONGEZWA KUPAMBANA NA UPOTEVU WA MAJI

Na Amon Mtega,Matuki DaimaAPP Songea.

MTENDAJI mkuu wa taasisi ya huduma za maji Nchini Tanzania (ATAWAS)Constantino Chiwaligo ameipongeza mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Songea  (Souwasa) Mkoani Ruvuma kwa kufikisha asilimia 21 dhidi ya mapambano na upotevu wa maji kwenye Wilaya hiyo.

 

 Chiwalo ametoa pongezi hizo mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema wakati akizindua mashindano ya michezo ya mpira wa miguu na mpira wa pete (MAJI CUP)kwa taasisi zilizo chini ya Wizara ya maji kwa kanda ya kusini ambayo ni rasmi kwaajili ya kuhumiza jamii utunzaji wa maji na vyanzo vyake.



 Mtendaji mkuu huyo amesema kuwa kwa upende wa utunzaji wa maji yasipotee ovyo mamlaka ya maji Songea imekuwa ya mfano hadi sasa inaasilimia 21 bado asilimia moja kufikisha malengo yaliyokusudiwa tofauti na mamlaka nyingine za maji hapa Nchini ambazo upotevu wa maji umekuwa mkubwa.


 Amefafanua kuwa baada ya Waziri wa Maji Juma Aweso kutambua kuwa kumekuwepo kwa baadhi ya mamlaka za maji kuwa na upotevu wa maji ndipo alikuja na mbinu ya kuanzisha mashindano ya michezo wa mpira yenye lengo la kufikisha ujue kwenye jamii namna ya kulinda na kuvitunza vyanzo vya maji.


 Kwa upande wake Mkurungenzi mhandisi Patrick Kibasa wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Songea (Souwasa) amesema kuwa katika bajeti ya mwaka huu wa fedha 2022/2023 imetenga fedha kwa ajili ya kutekeleza kazi mbalimbali ambazo utekelezaji wake unakusudia kupunguza kiasi cha maji yanayopotea kutoka wastani wa asilimia 21 (mwaka 2021/2022 )na kufikia asilimia 20 ifikapo Juni 2023.


 Mkurungenzi Kibasa akizungumzia mashindano hayo wakati akisoma risala kwenye uzinduzi huo amesema kuwa mashindano hayo yameshirikisha kanda ya kusini na kuwa timu zitakazo fuzu zitakwenda fainali ambayo itafanyika Mkoa wa Morogoro mwaka huu.


Naye mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema wakati akizindua mashindano hayo amesema kuwa mashindano hayo ni mazuri huku akiomba jamii ishirikishwe zaidi kwa kuwa ndiyo inayofanya shughuli za kibinadamu kwenye maeneo ya vyanzo vya maji.


Mkuu huyo katika hatua nyingine amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri wa Maji Jumaa Aweso kwa kazi kubwa ya kuhakikisha wanamtua ndoo mama kichwani kwa kutoa fedha mbalimbali kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji.

             






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI