Header Ads Widget

RC WA SIMIYU ATOA RAI KWA WAKULIMA

NA ZULFA KHALFAN ,MATUKIO DAIMAAPP,SIMIYU

Mkuu wa mkoa wa Simiyu dk. Yahaya Nawanda amewataka wakulima kutunza mazao waliyovuna msimu huu ili kuepukana na upungufu wa chakula kwa kuwa hawakupata mavuno ya kutosha



Ameyasema hayo wakati akihitimisha maonesho ya nane nane kanda ya ziwa mashariki yaliyofanyika katika viwanja vya nyakabindi wilayani Bariadi mkoani Simiyu ambapo ameeleza kuwa kutokana na upungufu wa mvua katika msimu wa kilimo wa 2021/2022, wakulima wahajapata mavuno ya kutosha hivyo wanapaswa kutunza mazao waliyonayo ili kuepuka njaa.

Aidha katika maonesho hayo jeshi la kujenga taifa (JKT) limekuwa mshindi wa kwanza kwa taasisi za serikali na mshindi wa tatu wa jumla katika maonesho hayo.

Akizungumza ushindi huo kanali George Kazaula mwakilishi wa mkuu wa jeshi la kujenga taifa amesema kuwa JKT ni wadau wa kilimo na uvuvi, na hiyo ndiyo siri kubwa ya ushindi huo na amewaomba wananchi kuendelea kutembelea katika maeneo ya mapando yao ili kujifunza zaidi.

Naye luteni kanali Mantage Kombe ambaye ni Mwenyekiti wa maandalizi ya nane nane kwa upande wa JKT Kanda ya ziwa mashariki, ameeleza kuwa wanandelea kuweka mikakati ambayo itawasaidia kuwa na mwendelezo wa ushindi katika maonesho mengine yajayo.

Maonesho hayo ya nane na Kanda ya ziwa mashariki yameanza agosti mosi na yatahitimishwa agosti 10 mwaka huu katika viwanja vya nyakabindi wilayani Bariadi mkoani Simiyu ambapo yamehusisha mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI