Header Ads Widget

"NISHAPOKEA ZAIDI YA WATOTO (3) WA MUME WANGU HADI SASA" DOREEN MREMA



Mjane wa aliyekuwa Mwenyekiti wa TLP Hayati Augustino Lyatonga Mrema, Doreen Mrema amesema kuwa hadi sasa ameshapokea watoto wa Hayati Mrema zaidi ya watatu (3) ambao walikuwa hawajatambulika kwenye Familia na ameahidi ataendelea kuwapokea na kuwalea kama mama yao na yupo Tayari kuendelea kuwapokea endapo tu ni kweli watakuwa ni watoto wa Mzee Mrema


Doreen amesema hayo jana wakati akizungumza na vyombo vya habari Mjini Moshi ambapo pia ametoa shukrani zake kwa viongozi wa Serikali, vyama vya siasa na watu binafsi kwa kuwa nao kipindi chote cha msiba.


"Alinieleza Nisiogope na niwapokee na niombe radhi kwenu, niwakumbatie na niwalee kama mama yao kama ambavyo yeye angewalea na ninamshukuru Mungu nimeendela kuwapokea watoto ambao walikuwa bado hawajambulika kwenye familia na sasa nimeshapokea zaidi ya watoto watatu (3). Mimi kama mama nitaendelea kuwapokea na kuwakumbatia kama ambavyo Mume wangu Mpenzi alivyoniasa siku 2 kabla ya kifo chake" - Mjane wa Mrema, Bi. Doreen Mrema 


Aidha amewahakikishia Watanzania kuwa ataendelea kumuenzi mume wake mpenzi (Hayati Mrema) na kuishi vile alivyomuasa na muda sahihi wakizungumza ukifika ataeleza ukweli juu ya maneno yanayoongelewa katika mitandao ya kijamii.


"Muda sahihi ukifika nitasema ukweli wote,yapo maneno mengi yanayo ongelewa na watu na mengine yameandikwa kwenye vyombo vya habari na mtandaoni,ila muda ukifika nitasema,siogopi na Mzee Mrema alisema nisiogope hata wakati hayupo"Doreen Mrema


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI