Header Ads Widget

TACRI YATOA MAFUNZO KWA WAKULIMA WA KAHAWA ZAIDI 6,000.

 



Na Amon Mtega ,Songea.


ZAIDI ya Wakulima 6,000 wa zao la Kahawa Mkoani Ruvuma wamepatiwa mafunzo ya ulimaji bora wa zao hilo ili liweze kuwaongezea kipato pindi wanaposhindana kwenye masoko ya ndani na nje.


Akizungumza kwenye siku ya nanenane Afisa ugani toka taasisi ya utafiti wa kahawa Tanzania ( TACRI)Victor Akulumuka amesema kuwa Wakulima hao wamepatiwa mafunzo na taasisi hiyo baada ya kubaini kuwa baadhi yao wamekuwa wakilima zao hilo kwa mazoea.


 Akulumuka amesema kuwa mafunzo hayo yamekuwa yakitolewa kwa wakulima hao kwa kupitia vyama vyao vya msingi (AMCOS) ambazo zimekuwa zikifanya kazi na wanachama wao na Wakulima.

 


  Afafanua kuwa licha ya kupatiwa mafunzo wakulima hao lakini bado TACRI imetoa mafunzo kwa wakulima viungo zaidi ya 300 ambao hao hutumika kama maafisa ugani kupita kuwasaidia baadhi ya wakulima ambao hawakupatiwa mafunzo hayo pindi wanapopanda miche ya zao hilo.


 Akizungumzia ufanyaji kazi wa taasisi hiyo amesema kuwa katika kipindi cha mwaka jana 2021 taasisi hiyo ilizalisha miche ya kahawa Milioni  2.3  na kuwa katika msimu wa mwaka huu taasisi hiyo imejipanga kuzalisha miche zaidi ya Milioni 2.5 ili kukidhi mahitaji ya wakulima wa zao hilo.


 Amesema kuwa miche inayozalishwa na taasisi hiyo ni aina ya kahawa ya Arabika ambayo inadaiwa kuwa ni  bora na haishambuliwi na magonjwa na kuwa wakulima wakizingatia maelekezo ya wataalam pamoja na mafunzo wanayopatiwa  mara kwa mara  basi watafanikiwa kuwa na kahawa bora ambayo kila mche mmoja  hutoa kilo tano hadi sita tofauti na miche mingine ambayo haina ubora.


 Hata hivyo mtafiti huyo amevipongeza vyama vya msingi AMCOS ambazo hufanya kazi na Wakulima wake hasa Amcos ya Kimuli iliyoko Mbinga mjini na Amcos ya Mahenge iliyoko Mbinga Vijijini kata ya Litembo.


         


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI