Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani imetenga fedha shilingi milioni mia tano kwa ajili ya uje zi wa jengo jipya ili kuongeza ufanisi kwa kutoa huduma kwa wananchi.
Hayo yalisemwa na mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Shauri Salenda katika kikao cha baraza la madiwani robo ya nne ya mwaka 2021/2022 baada ya mhadisi wa halmashauri hiyo kuwasilisha ramani ya mchoro wa jengo jipya mbele ya madiwani,wakuu wa ifara na wadau mbalimbali waliohudhuria kikao.
"Halmashauri yetu imetenga fedha shikingi milioni 500 ambazo zitaanza ujenzi kwa ajili ya watumishi kupata mazingira rafiki na wananchi kurahisisha kutoka sehemu moja hadi nyingine kufuata huduma ili huduma zote ziweze kupatikana sehemu moja."Alisema Selenda .
Pia aliongeza kuwa kwa sasa majengo yaliopo hapa halmashauri yanatumika na baadhi ya idara zipo katika maeneo mengine na kuzitaja idara hizo kuwa ni elimu,ardhi na sheria ambazo lazima wananchi wazifuate mbali na hapa.
Alisema kuwa haya ni maendeleo naamini tutaanza ujenzi hata kama sitalimaliza watalimaloza wengine wananchi wa Bagamoyo ni fahari kuwa na jengo jipya mji huu unakuwa kila siku nawaomba tltue delee kushirikiana ili kuwatumikia wananchi wa Bagamoyo na kuacha alama kwa vizazi vijavyo kama wazee wetu waliotangulia na kuanzisha halmashauri hii.
Akiwasilisha mchoro huo mhandisi wa Halmashauri hiyo Wilton Martine alisema jengo hilo linatarajia kuwa na ghorofa tatu ambazo kwa mpangilo wake utakuwa ba idara zote na kwa ufanisi zaidi.
Awali katika kikao hicho mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mohamed Usinga alisema kwa muda wamekuwa wanampango wa kuboresha majengo hivyo umefika wakati halmashauri hiyo kupata jengo jipya katika eneo la ukuni kata ya Dunda.
0 Comments