Na Gabriel Kilamlya ,Matukio DaimaAPP Njombe
BARAZA la madiwani Halmashauri ya Njombe limesema linafanyia kazi Malalamiko ya ushuru wa mazao ya misitu zikiwemo Mbao .
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Valentino Hongoli amesema kuwa malalamiko ya gharama kubwa ya ushuru wa mbao kwa wafanyabiashara wa mazao ya misitu yamefanyiwa kazi kwa kushusha toka shilingi 200 hadi shilingi 100.
Katika mkutano wa baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Njombe Bwana Hongoli ametumia fursa hiyo kuwaalika wafanyabiashara kurejea kufanyiabiashara hiyo ndani ya halmashauri hiyo kwani vikwazo vimeondolewa.
Awali ushuru wa shilingi 200 kwa kila ubao ndani ya halmashauri hiyo ulisababisha wafanyabiashara wengi kuibua malalamiko makubwa na wengine kuhama kufanyabiashara katika eneo lao Jambo lililosababisha kushuka kwa mapato ya ushuru wa mbao kutonana na sheria zilizotungwa.
Kutokana hatua hiyo Bwana Hongoli ameelekeza kufungwa kwa kamera za CCTV kwenye mageti makubwa ambayo yanapitisha idadi kubwa ya mazao ya misitu kwa lengo la kudhibiti mianya ya utoroshaji mapato.
Aidha amewaonya watendaji wa vijiji na kata wenye tabia ya kukubaliana na wafanyabiashara kutorosha mapato na kwamba watakaokamatwa adhabu kali zitachukuliwa dhidi yao.
0 Comments