Ushahidi kutoka kwa mwanaharakati anayepambana na ufisadi nchini Kenya, John Githongo, kuunga mkono madai ya mgombea urais Raila Odinga, kwamba mfumo wa matokeo ya uchaguzi ulidukuliwa ili kumpokonya ushindi unashabihiana na waraka uliowasilishwa mwaka wa 2017.
Miaka mitano iliyopita, Bw Odinga pia alipinga matokeo ya uchaguzi na Mahakama ya Juu ikaamuru urudiwe.
Kurasa nyingi za waraka wa 2017 zinazoonyesha kumbukumbu - neno la kiufundi kwenye mfumo wa kompyuta - zinaonekana kuwa sawa na zile zilizo kwenye hati ya sasa, wakati mwingine na tarehe tu zimebadilishwa.
Picha za skrini katika hati ya kiapo iliyowasilishwa na Bw Githongo na kuripotiwa kutoka kwa mtoa taarifa hata mwaka wa 2017 zipo miongoni mwa tarehe zilizokusudiwa kuwa za Agosti mwaka huu.Pia kuna makosa ambayo yanaonekana kwa urahisi kwa mfano, muda uliotolewa kama 16:54:30(saa kumi na dakika hamsini na nne na sekunde thelathini) jioni katika hati ya 2017 unaonekana kama 6:54:30 (saa kumi na mbili dakika hamsini na nne na sekunde thelathini) jioni katika wasilisho lililotolewa wiki hii, ambayo inaonekana kukosa tarakimu ya kwanza.
0 Comments