Na Gabriel Kilamlya NJOMBE
Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka Amesema anataka kuimarisha sekta ya Michezo kwa kuanza kuwekeza kwa kuandaa ligi za watoto wanaotokana na UMITASHUMTA NA UMISETA Ili kuwapata vijana watakaofundishwa mpira tangu wadogo.
Mtaka Ametoa kauli hiyo wakati akifunga mashindano ya ligi ya Ndondo ya Kuambiana Cup yaliyoandaliwa na mkazi wa kata ya masasi wilaya ya Ludewa bwana Iman Haule ambaye ni mkurugenzi wa Kampuni ya Kuambiana Investiment Ltd.
Awali mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga Amesema Ataendelea kuwa bega kwa bega na Wadau mbalimbali wa michezo wanaoanzisha ligi katika jimbo lake kwani watu wake wanapenda sana michezo.
Ilela FC Imechukua ubingwa wa ligi hiyo kwa kumchabanga Kipangala fc magoli 3 kwa 1 na kujinyakulia kitita cha fedha kiasi cha shilingi Laki Tano,Seti ya Jezi,Mpira na Kombe.
0 Comments