MAKAMO wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mh. Othman Masoud Othman amekuwa miongoni mwa viongozi wa juu waliosajiliwa kwa ajili ya Ushiriki wa mbio za Kimataifa za Zanzibar zinazofahamika Tigo Zantel International Marathon,
Mh.Masoud amesajiliwa na Kamati ya mbio hizo, mapema leo ofisini kwake migombani,Visiwani Zanzibar.
Aidha, Kamati hiyo pia imeweza kumsajili Makamo wa Pili wa Rais, Mh.Hemed Suleiman Abdullah,
Pia imewasajili Kamishna wa Police Zanzibar (CP) Hamad Khamis Hamad, Ofisini kwake na Kamanda wa KMKM.
Kamati hiyo, pamoja na mambo mengine iliweza kuwajulisha viongozi hao, kuhusu matukio yote yatakayofanyika siku ya Tarehe 5 na 6 katika ufukwe wa Mercury (Mizingani Road) na pia siku ya Marathon tarehe 7, itakayoanza kuanzia saa 12 za asubuhi.
Kamati hiyo pia anaendelea na usajili kwa viongozi na wengineo huku pia zoezi la kujisajili likiendelea katika vituo mbali mbali vilivyopo Dar es Salaam katika maduka ya
Just Fit Mlimani City na Kijitonyama kwa waliopo Dar es salam na walio Zanzibar zoezi la usajili linaendelea katika jengo la Michenzani Mall, Mgahawa wa Mercy na Catalunia- Kiembe samaki au kwa njia ya kielectroniki kupitia App ya (Nilipe) au kwa Lipa namba 5121222 kutoka kwenye mtandao wako wowote." Ilieleza taarifa hiyo ya Kamati ya mbio.







0 Comments