NA ARODIA PETER, MATUKIODAIMAAPP APP DAR
MBUNGE Mstaafu wa Jimbo la Kilwa Kusini, Suleiman Bungara maarufu Bwege, yupo njiani kuelekea nchini Kenya kumpigia kampeni mgombea Urais wa Ushirikiano wa Azimio la Umoja, Raila Odinga.
Bwege ambaye pia amepata kugombea Ubunge wa Jimbo hilo kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo kwenye Uchaguzi Mkuu 2020 hotuba zake zimekuwa zikiwavutia Wakenya tangu akiwa mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Taarifa ya ACT Wazalendo iliyotolewa na Naibu Katibu Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, Janeth Rithe leo Agosti 4 mwaka huu imesema, Ndugu Bwege ndio Mwanasiasa wa kwanza kutoka Tanzania kupewa heshima hiyo na Timu ya Kampeni ya Azimio la Umoja.
"Kumbukumbu za mtandaoni zinaonesha kuwa hotuba za Ndugu Bwege ndani na nje ya Bunge zimekuwa zikifuatiliwa sana na kupendwa zaidi nchini Kenya." imesema sehemu ya taarifa ya chama hicho
Mwisho
0 Comments