Header Ads Widget

LIMENI VIAZI LISHE KUBORESHA AFYA-TARI

  

Na Matukio DaimaAPP,Mtwara

Taasisi ya Kilimo Tanzania Tari kituo cha Naliendele imewahamasisha wakulima wa viazi lishe  kutoka kanda hiyo kuhakikisha kuwa wanalima kwa wingi ILI kuboresha afya zao. 


Aidha mtafiti huyo alisema endapo watalima kwa wingi wanaweza  kupata fursa ya kusindika zao hilo na kupata juice ambayo inaweza kutumika kama kinyawaji wakati ambao umeshavuna.


Kauli hiyo ameitoa Mtafiti wa zao la viazi kutoka Taasisi ya Kilimo Tanzania Tari kituo cha Naliendele Bernadetha Kimata alipokuwa akiongea katika maonyesho ya nanenane yananayofanyika wilaya  Lindi katika viwanja ngongo,


Alisema wakulima na wadau wa kilimo wafike katika banda  hilo ili kujifunza katika kipindi maalum cha wananchi kujifunza teknolojia mbalimbali katika darasa maalum”


“Unapokula viazi lishe vile vyenye rangi iliyokolea unapata vitamin A ambayo ni muhimu kwenye mwili lakini pia ina saidia kupunguza tatizo la watu kuona na kuacha kutumia miwani”


"Katika jambo zuri ambalo wakulima wanapswa waelimishwe ni upandaji wa viazir lishe ulivyo rahidi ambapo ndani ya miezi minii 4 unavuna hivyo unaweza panda kwakuoshanisha 


"Unajua viazi lishe vinastawi kwenye udongo tifutifu wenye rutuba ya kutosha na unaoruhusu maji kupenya kwa urahisi  lakini udongo mfinyanzi nawenye kokoto nyingi haufai kwakuwa unazuia mizizi kupenya na kupanuka"


"Viazi hustawi maeneo yenye mwinuko chini ya mita 1700 kutoka usawa wa bahari  na pia huitaji joto la kati ya nyuzi joto 15-30 pia huitaji mvua ya wastani wa milimita 600 kwa mwaka"


"Zipo aina mbalimbali za viazi ambapo unaweza kuchagua mbegu kulingana na kanda ulipo kwa kanda ya pwani unaweza kutumia aina tano zinazo faaambazo ni mataya, ukerewe, kiegea, chahwa,  na simama"

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI