Header Ads Widget

DC WA TANDAHIMBA APONGEZA TAASISI YA TARI

 


Na Matukio DaimaAPP, Lindi

 Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Kanal Patrick Sawala  ameipongeza Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania Tari kituo cha Naliendele kwakufanyakazi nzuri yenye matokeo sahihi yenye tija kwa wakulima nchini. 


Kauli hiyo ameitoa wakati alipotembelea banda la taasisi hiyo lililopo katika maonyesho ya nanenane Ngongo mkoani Lindi ambapo amesisitiza wakulima kufika katika taasisi hiyo na kujifunza fursa zilizopo kwaajili ya maendeleo ya taifa. 


“Tari wanafanyakazi nzuri katika utafiti wa mbegu na magonjwa mbalimbali na jinsi wanavyoongeza thamani ya mazao yetu tumeona mbegu nzuri za mafuta kama ufuta, karanga, alizeti na mawese hii taasisi inafanyakazi kubwa kwa taifa” 


“Unajua kwenye mbali na kuuza korosho ghafi na korosho karanga tumeona wakitengeneza wine spirit juice na wine inaweza kuwa dry ama sweet  lakini tumeona bidhaa za korosho nyingi natoa wito wakulima watanzania waje kujifunza kuongeza maarifa ili kilimo kiwe kilimo biashara kwelikweli”


“Ukija Tari utaona namna gani wanaweza kufanya kazi kubwa katika uongezaji wa thamani wa mazao hasa kwenye korosho ambao unavutia uige ili wakulima waweze kunufaika na zao hilo ambapo huuza zikiwa ghafi wanauza kwa bei ya hasara lakini wakiongeza thamani wanaweza kupata faida kubwa na kuliingizia taifa mapato yatokanayo na zao hilo” alisema Kanal Sawala 


"Tandahimba ndio wazalishaji wakubwa wa korsho Tanzania baada ya kufika hapa tutegemee kuongeza makusanyo mengi ya korosho kwakufanya kazi kwa ukaribu na tari hata mashamba mengi darasa ya korsho ya tari yapo tandahimba"


"Wamekuwa wakitoa elimu mbalimbali kwa wakulima ambapo wanafundishwa niwape moyo kazi mnayofanya ni kubwa sisi viongozi tunatamani kila mkulima apate mbegu bora inayozaa mazao mengi yenye kwa mkulima"


"Serikali inasisitiza ulimaji wa mazao yanayotoa mafuta kwa wingi ili kuweza kupata mafuta mengi watanzania nunueni mbegu zilizofanyiwa utafiti na taasisi hiii ili kuipunguzia serikali gharama kubwa ya kuagiza bidhaa hiyo" alisema Sawala 

MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI