Header Ads Widget

KINYOZI AFUNGWA JELA MIAKA 30 KUMPA MIMBA MWANAFUNZI WA MIAKA 18

 


Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemuhukumu kifungo cha miaka 30 Batista Ngwale (27) kwa kukutwa na hatia ya kumpa mimba Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 18 ambaye alikuwa akisoma kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Kibena iliyopo Iringa vijijini. Na MatukioDaimaAPP,Iringa


 Batista alikuwa akijishughulisha na kazi ya kinyozi ambapo ameiomba Mahakama kumpunguzia adhabu kwasababu ana Ndugu watatu na Mtoto mmoja ambaye anasoma Shule ya awali ambao wote wanamtegemea, maelezo ya Mahakama yanaeleza kuwa Kijana na Binti walifanya mapenzi mara mbili vichakani huku Kijana akijua dhahiri kwamba Binti huyo ni Mwanafunzi.  


Kesi hiyo ilikuwa na Mashahidi sita akiwemo Daktari wa kituo cha afya cha Ifunda ambapo Binti alipelekwa kufanyiwa uchunguzi na kugundulika ana ujauzito wa wiki nne, Shahidi wa tatu ni Binti ambaye ameiambia Mahakama kuwa walianza mahusiano na Batista Mwezi May na walijamiana Mwezi June na baada ya mwezi mmoja alijihisi mjamzito na alimtaarifu Mhusika na akamshauri watoe lakini Binti hakutaka kutoa mimba hiyo na siku alipofi mahakamani kutoa ushahidi alikuwa mjamzito .


Kesi hiyo imesimamiwa na mawakili wa Serikali Radhia Njovu ,Simon Nashon pamoja na Reuben Lubango ambapo waliiomba mahakama kutoa adhabu Kali  Kwa sababu kitendo hicho Cha kufanya mapenzi kichakani kinafedhehesha mwanamke .


Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi mkuu wa Said Alli Mkasiwa kuwa Kwa kuzingatia athari za kukatisha masomo ya mwanafunzi huyo mahakama inamhukumu kifungo Cha miaka 30 jela kijana huyo .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI