Yohana Mwila, mchezaji wa Tanzania mchezo wa kunyanyua vitu vizito kwa walemavu (Para Powerlifting) katika michezo ya Jumuiya ya Madola akishiriki mashindano hayo kwenye ukumbi wa NEC jijini Birmingham, Uingereza, ambapo hakushinda.
Hata hivvyo pamoja na kushindwa kutwaa medali medali lakini Mwila ame Qualify kwenda kushiriki kwenye michezo ya Para Olympic mwaka 2024 jijini Paris,Ufaransa.
Mwila, mwenye umri wa miaka 38 na ambaye ni mara yake ya kwanza kushiriki mashindano makubwa alivunja rekodi yake mwenyewe ya uzito wa kilo 130 na kubeba kilo 136, ambapo kiwango cha uzito kwa Olimpiki ni kilo 135.
Mwila, anayecheza uzito wa Lightweight kilo 59-65 alibeba 130-135-136 katika attempt zake tatu bila kupoteza pointi, alisikitika kwamba kwenye mashindano hayo washindani wa uzito tofauti ikiwemo uzito wa juu Heavyweight kilo kuanzia kilo 89 kuendelea kuchanganywa na wao wa uzito mdogo, sababu ikielezwa kuwa ni upungufu wa washiriki, ambao jumla walikuwa tisa na kila mtu na category yake.
Mshindi alikuwa B. Gustin kutoka Malaysia aliyebeba kilo 210-216-220 katika attempts zake tatu huku uzito wake ni kilo 69.50.
0 Comments