Header Ads Widget

KANALI AHMED ABBAS RC, MTWARA AIPONGEZA TPDC

 





NA HADIJA OMARY_ LINDI.



MKUU wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas  amepongeza jitihada zinazofanywa na Shirika  la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)  hususani kwenye shughuli za utafiti na uendelezaji wa nishati ya mafuta na gesi asilia nchini.



Kanali Abbas ametoa pongezi hizo alipotembelea banda la  Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)


Katika Maonesho ya Nane nane yanayoendelea katika viwanja vya Maonyesho hayo Ngongo Manispaa ya Lindi Mkoani humo.




Aidha sambamba na miradi ya usambazaji wa gesi asilia majumbani Mhe Ahmed amepongeza TPDC kwa jinsi inavyowajibika kurudisha kwa jamii (CSR) ikiwa ni pamoja na  kutekeleza miradi mbalimbali ya kijamii kwenye sekta ya  elimu, afya ,maji na utawala bora kwa mikoa ya Pwani, lindi na Mtwara. 




"Tunaipongeza TPDC kwa kua imara kwenye utekelezaji wa miradi ya utafiti, uendelezaji na usambazaji wa gesi asilia nchini, vilevile tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita ya Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuunga mkono miradi ya gesi asilia nchini ikiwemo mradi mkubwa wa kusindika gesi asilia kuwa kimiminika (LNG ) ambao utajengwa mkoani Lindi wenye thamani ya Shilingi Trilioni Sabini (70) " alisema kanali Ahmed. 



Aidha kanali Ahmed pia amepongeza jitihada zinazofanywa na Shirika hilo katika kuelimisha jamii huku akisisitiza kuendelea kutoa elimu kwa umma ili miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa nchini ifahamike kwa wananchi.  



Kwa upande wake Ofisa Maendeleo ya jamii wa TPDC Oscar Mwakasege alieleza juu ya faida za matumizi ya gesi asilia nchini ikiwa ni pamoja na kuimarika kwa uzalishai wa umeme ambapo asilimia 62% ya umeme nchini ni wa gesi asilia,  kuongezeka kwa matumizi ya gesi asilia majumbani na kwenye magari 



ambapo hata hivyo alieleza kuwa  hadi sasa kunamagari 1400 yanayotumia gesi asilia badala ya mafuta na  nyumba 1500 zinatumia gesi asilia na kwa mwaka wa fedha 2022/23 kwa mkoa wa Lindi kata ya Mnazi mmoja  nyumba 200  zitaunganishwa kutumia gesi asilia.




Aidha Serikali imeweza kuokoa fedha za kigeni kwa kutumia gesi asilia katika uzalishaji badala ya mafuta ambapo  kiasi cha dola za kimarekani Bilioni 17.7 sawa na Shilingi Trilioni 40.15 kimeokolewa.


Ikiwa ni muendelezo wa shughuli za utafiti wa mafuta na gesi asilia nchini, 



Nae Mhandisi wa Mafuta na Gesi Lessa Simoni alisema kuwa TPDC inaendelea na utafiti katika bonde la Eyasi Wembere ambalo linagusa mikoa ya  Arusha,  Singida, Shinyanga, Simiyu na Tabora.



 Lessa alieleza kuwa hatua ya sasa ya utafiti ipo katika ukusanyaji wa takwimu  za kijiokemia ili  kuangalia uwepo wa uvujaji wa mafuta kwenye miamba ambapo inatumika  teknolojia ya uwekaji  wa moduli  (Amplified Geochemical Imaging).



  Amesema kitalu hicho cha Eyasi Wembere kinafanana sifa zake za kijiolojia na vitalu vya nchi jirani ya Uganda na Kenya ambapo wamegundua mafuta hivyo inatoa hamasa kuwa na uwezekano mkubwa wa kugundua Mafuta au gesi katika Maeneo hayo. 



Akizungumzia miradi ya mingine ya utafiti inayoendelea Mhandisi Lessa amesema katika Mradi wa Mnazi Bay Kaskazini (North) na Songosongo (west) Magharibi wanaendelea na maandalizi ya kuchimba vizima vya utafiti wa mafuta na gesi asilia.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI