WAKATI Rais Samia Sulua Hassan anataraji kuanza ziara yake Agosti 11 mwaka huu katika mkoa wa Iringa,kamishna wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC ) mkoa wa Iringa Daud Masasi amesema amemwandikia Rais barua ya wazi yenye mambo makuu matano kama sehemu ya kutambua jitihada za serikali ya awamu ya sita na kumshauri kufanyia kazi mambo hayo aliyoandika kwenye barua hiyo.
Akizungumza na wanahabari leo mjini Iringa Masasi alisema kuwa barua hiyo aliiandika toka Mei 16 mwaka huu na kuwa jambo la kwanza alilimwandikia Rais Samia kwenye barua ni hiyo ni juu ya Lugha adhimu ya Taifa Kiswahili kuhakikisha chati ya kuwa miongoni mwa lugha kuu ya dunia kwa kuona kiswahili kinatendewa haki na hatua zinachukuliwa kulinda,kuendeleza lugha hiyo.
Masasi ametaja jambo la pili katika barua hiyo ni suala la utamaduni na michezo kuwa utamaduni mambo hayo ni msingi sana katika Taifa kwa maana ya Lugha ,mavazi , chakula ,ngoma za makabila ,mila na destuli na mengine na msingi bora wa Taifa ,jambo la tatu ni ardhi na kilimo wakati jambo la Nne katika barua hiyo ni majina ya mikoa na mwisho ni kuufanya mkoa wa Iringa kuwa na hadhi ya muonekano wa jiji.
" kama miji mingi nchini imekuwa kwa kasi na idadi ya watu inaongezeka sana katika mji wa Iringa panaitwa Miyomboni enzi hizo kulikuwa na miti hiyo aina ya miyombo wakati kata ya Kitanzini jina la makumbusho ya kitanzi kilichotumika kunyongea watu kipindi cha wakoloni na ndioa eneo lenye maduka na shughuli nyingi za kila siku" alisema
Kuwa wafanyabiashara wenye maduka asilimia 99 wana vyombo vya usafiri lakini watu wengine wanalazimika kufika katikati ya mji huo wa Iringa kwa usafiri ila wanakosa maeneo ya kuegesha magari yao na kama mji utapewa hadhi ya jiji ni wazi maeneo ya maegesho yataboreshwa zaidi.
Pia alisema kwa sasa ni wakati muafaka wa soko kuu la Iringa ambalo ni la miaka mingi sana kuboreshwa maana soko hilo ni la enzi za mkoloni miaka ya 1960 hivyo limechoka .
Masasi alisema jambo kubwa zaidi ni kuufanya mji wa Iringa kuwa na sura ya kivutio kwa kuona mji huo unajengwa kisasa zaidi ili kuendelea kubaki kuwa lango la utalii wa nyanda za juu kusini na kuhakikisha eneo la Gereza la Iringa mjini linahamishwa kwenda nje ya mji huo eneo la Mlolo.
" Mheshimiwa Rais Samia , Iringa City inafaa kujengwa eneo hilo la gereza la Iringa ambalo kwa sasa lipo mjini kabisa na ndugu zetu wa gereza wanaweza kuhamishiwa maeneo mengine mengi yaliyopo nje ya mji na huko kupata nafasi nzuri na kubwa ya kujenga gereza na kufanya shughuli za uzalishaji tofauti na sasa "
Hata hivyo Masasi amepongeza jitihada kubwa za kiubunifu zinazofanywa na Rais Samia katika kutangaza utalii kupitia The Royal Tour kuwa ni ubunifu mkubwa wenye tija kwa sekta ya utalii na uchumi wa nchini .
Wakati huo huo Masasi amepongeza upanuzi wa uwanja wa Ndege Iringa (Nduli) kuwa utachangia kwa kiasi kikubwa kukuwa wa setika ya utalii katika mkoa wa Iringa kwa kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea hifadhi ya taifa ya Ruaha.
Pia kuhusua suala la ruzuku ya Mbolea ambalo Rais Samia ametangaza kuanza mapema mwezi huu alisema ni jambo kubwa ambalo litaongeza kasi ya uzalishaji kwa wakulima wa mkoa wa Iringa na Taifa .
Katika hatua nyingine Masasi aliwataka watanzania kuepuka kushawishika na baadhi ya wanasiasa wasio na nia nzuri kwa Taifa ambao wanataka kupotosha juu ya zoezi la sensa ya watu na makazi na kuwa suala la sensa ya watu na makazi ni la taifa na kila mmoja anapaswa kushiriki katika zoezi hilo Agosti 23 mwaka huu.
0 Comments