Na Amon Mtega _Songea
DIWANI wa kata ya Mjini Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma Mathew Ngalimanayo amewataka wakazi wa kata hiyo kushiriki kikamilifu zoezi la Sensa Augost 23 mwaka huu ili kuendana sambamba na mpango wa Serikali wa kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Wito huo ameutoa wakati akiwahutubia mamia ya wakazi wa kata hiyo kwenye mkutano wa hadhara ambao uliandaliwa na diwani hiyo kwa lengo la kuwahamasisha wananchi kushiriki zoezi la sensa.
Ngalimanayo akizungumza kwenye mkutano huo amesema kuwa Serikali inapopanga bajeti kwaajili ya kuwahudumia Wananchi wake ni lazima iwe na takwimu sahihi za watu wake ,hivyo kunakilasababu za kuhakikisha Wananchi wanashiriki suala la sensa.
Aidha katika hatua nyingine diwani huyo ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kuhakikisha miradi ya sekta mbalimbali mbalimbali inatekelezeka ikiwemo ya kwenye kata hiyo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Songea mjini Hamis Abdallah Ali amesema kuwa Serikali imekuwa ikifanya mambo makubwa ya kimaendeleo hivyo ni vema kila mwananchi akatambua maendeleo hayo kwa kuunga mkono kazi hizo.
Mwenyekiti huyo licha ya kuwataka Wananchi watambue kazi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan lakini bado amempongeza diwani wa kata ya Mjini Mathew Ngalimanayo kwa kuweka mkutano huo wa kuwaeleza Wananchi manufaa ya sensa.








0 Comments