SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema itamchukulia hatua mwananchi yeyote ambae atakutikana anafanya biashara ya mchanga kwasababu Wizara ya Maji, Nishati na Madini (WMNM) imeshatoa elekezo katika ununuzi wa maliasili hiyo kwamba wananchi wanatakiwa kufanya manunuzi kwa njia ya mfumo.
Akizungumza na waandishi wa habari Naibu Waziri wa Maji, Nishati na Madini Mhe Shaaban Ali Othman wakati akitoa taarifa ya ufunguzi wa shimo jipya la mchanga katika ukumbi wa jengo la ZURA alisema uuzaji wa maliasili zisizorejeshaeka unafanywa na Serikali na sio mwananchi. Hivyo hatuka kali za sheria zitachukuliwa kwa atayefanya biashara ya mchanga Zanzibar.
Mhe. Othman alisema SMZ imeweka utaratibu maalum wa kufungua na kufuanga mashimo ya mchanga na wananchi wanatakiwa kununua kupitia tovuti https://madinismz.go.tz/ huo ndio utaratibu ambao umewekwa kwa wanaanchi wenye mahitaji ya mchanga kwaajili ya ujenzi na sio kupitia kwa mtu binafsi.
Alisema Wizara ya Maji, Nishati na Madini (WMNM) siku ya Julai 12, 2022 inafungua shimbo jipya la mchanga eneo la Bwimbuni Misufini la familia ya Bw. Juma Mwinyi liliyopo Wilaya Kaskazini ‘B” Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa ajili ya matumizi ya wananchi.
“WMNM inafungua shimbo jipya la mchanga eneo la Bwimbuni Misufini la familia ya Juma Mwinyi na inafunga shimo la ndugu Asha Ibrahim liliopo Donge Mchangani ambalo lilikuwa likitumika kwa matumizi ya kawaida ya wananchi’ Alisema Naibu Waziri huyo.
Alifahamisha bei elekezi kwa tani moja (1) ya mchanga ni shilingi elfu kumi (10,000) ambayo elfu saba 7,000 zitalipwa kupitia akaunti ya Wizara na elfu tatu (3,000) italipwa kwa akaunti ya mwenye shamba. Hivyo wananchi wasinunua maliasili hiyo kwa watu ambao wanafanya ulanguzi.
Aidha akijibu suali la muandishi aliyeta kujua sifa ya kufungua shimo la mchanga, Mhe Othman alisema sifa ziko nyingi lakini kati ya sifa hizo moja wapo shamba linatakiwa liwe halali kwa mmliki na baada ya hapo wataalum wanafanye tathmini lisiwe karibu na bahari, makaburi wala katika eneo la hifadhi ya misitu.
0 Comments