Header Ads Widget

WAZIRI MKUU KUSHIRIKI KOROSHO MARATHON MTWARA

  


Mtwara, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajia kushirii katika mbio za Korosho marathoni  zitakazo fanyika mkoani mtwara. 


Mbio hizo ambazo zitakuwa na washiriki zaidi ya 1200 kutoka maeneo mbalimbali ya nchi zikiwa na lengo la kutangaza fursa mbalimbali ambazo zipo kwenye zao la korosho hususani ubanguaji. 


Akizungumza kuelekea mbio hizo Kaimu Mkurugenzi Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Francis Alfred alisema kuwa mbio hizo zinalenga kutangaza tasnia ya korosho nchini na fursa za ubanguaji ili kuongeza kasi ya ubanguaji wa korosho nchini.


Alisema kuwa mbio hizo zitaongeza hamasa na kutangaza korosho kwakuunga mkono vikundi mbalibali vya ubanguaji wa korosho. 


“sisi tumejipanga na tumepata wadhamini wengi ambao watawezesha washindi kupata zawadi lakini pia pesa hizo kutumika kwaajili ya vikundi vya ubanguaji”


Nae Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya korosho marathoni Domina Mkangara alisema kuwa wanamtwara wanapaswa wajitokeze kwa wingi kuunga mkono mbio hizo ambazo zitaongeza hamasa ya ubanguaji wa korosho.


“Korosho ina fursa nyingi za uwekezaji tunapointangaza tuna maanisha kuwa ni ajira ambayo inasaidia watu wengi tujikite katika unanguaji tukiwa tunafanya mazoezi kwa afya”  alisema Domina 


Nae Benedicta  Mshanga Meneja Biashara kutoka benki ya CRDB kanda ya kusini alisema ambaye ni moja kati ya wadhamini alisema kuwa mazoezi ni afya na ulaji wa korosho ni afya pia tunapokuwa na wateja wenye afya njema kwa kufanya mazoezi inaongeza hamasa ya utendaji kazi.


“Ili tuendelee kutoa huduma bora tunahitaji taifa lenye afya njema ndio maana tushiriki katika mbio hizo kama wadhamini ili kuhakikisha kuwa tunaunga mkono juhudu za CBT kuhamasaisha vikundi vya ubanguaji ambavyo kwa namna yoyote ile wanaweza kuwa wateja wetu kwa kuweka pesa ama kwakukopa kwaajili ya kukuza mitaji ya bishara zao”alisema Mshanga 


Nae Meneja wa kampuni ya BENS Franki Mitti alisema  kuwa ili kupata mashamba bora wakulima wanapaswa kutumia viwatilifu sahihi katika mashamba yao.


“Mbio hizi zikawakumbushe wakulima kuwa ili kupata korosho bora za kubangua hawana budi kutumia viwatilifu sahihi katika mazao yao ndio maana tumeunga mkono ili kuwakumbusha wakulima tunaamini kuwa ubanguaji utaongezeka nchini” alisema Mitti


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI