Header Ads Widget

MBUNGE WA JIMBO LA MOSHI VIJIJINI PROF PATRICK NDAKIDEMI AANZA ZIARA KATA YA URU SHIMBWE

 


NA WILLIUM PAUL, MOSHI.


Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi ameanza ziara katika Jimbo lake ambapo alitembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika kata ya Uru Shimbwe.


Mbunge alijionea ujenzi wa kituo cha Polisi cha kata ambacho kinajengwa kwa nguvu za wananchi, pamoja na wadau wa maendeleo wa ndani ya nchi pamoja na kutembelea kituo Cha Afya Shimbwe ambapo alijionea na kuelezwa changamoto mbali mbali zinazokikabili kituo hicho.



Aidha alitemebelea shule ya Sekondari Shimbwe ambapo alikagua majengo ya shule yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi na wafadhili, Majengo hayo ni pamoja na jengo la utawala, madarasa, bwalo la chakula, hostel ya wasichana, pamoja na ujenzi wa choo cha wavulana.


Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Shimbwe, Mathew Felix amesema kuwa shule ina jumla ya  walimu 11 na wanafunzi 300 huku kukiwa na upungufu mkubwa wa waalimu wa masomo ya baiolojia, fizikia na hisabati. 



Pia shule hiyo ina changamoto ya umeme na  madarasa chakavu ambapo mwaka wa fedha 2021/2022 walipata kiasi cha shilingi milioni 57,500,000 kuendeleza jengo la utawala kutoka Serikali kuu. 


Mkuu huyo wa shule alieleza kuwa shule ina hosteli inayoendeshwa na wazazi kwa ajili ya wasichana na  ina uwezo wa kulaza watoto 86.



Mbunge alipata nafasi ya kutembelea kituo cha afya Shimbwe ambapo alielezwa changamoto zinazowakabili kama vile ukosefu wa chumba cha upasuaji, vifaa vya kupima choo kubwa,  ultra sound, x-ray na jenereta ya umeme wa dharura. 


Akiwa katika mkutano wa hadhara katika Ofisi ya Kijiji cha Shimbwe Juu, mbunge  
aliwapa wananchi mrejesho wa mambo makubwa yaliyopitishwa na bunge la bajeti ikiwepo ongezeko kubwa la bajeti ya wizara ya kilimo na uamuzi wa serikali kutoa elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita.  



Mbunge alipata fursa ya kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika sensa ya watu na makazi itakayofanyika 23/08/2022.


Katika mkutano huo, bunge alimshukuru  diwani wa kata hiyo, Bertin Mkami na wadau wa maendeleo wanaosaidia  kata hiyo kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta za Afya, Maji, Ulinzi na Elimu. 



Kwa kutambua juhudi za wananchi, Mbunge alikichangia kikundi cha ngoma za asili  cha akina mama wa Shimbwe Juu  kiasi cha Shilingi laki tano ili wanunue vifaa kwa ajili ya kikundi chao pamoja na mifuko 50 ya saruji kuunga mkono juhudi za wananchi kwenye ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Shimbwe Juu.

Katika ziara hiyo mbunge aliambatana na watalamu wa barabara kutoka TARURA na TANROADS ambao walitoa ufafanuzi kuhusu miradi ya barabara inayotekelezwa katika kata ya Uru Shimbwe.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI