Header Ads Widget

KCBL YAPATA FAIDA YA MIL. 318 KWA MARA YA KWANZA

 


Na Esther Machangu_Moshi.


Benki ya Ushirika ya KCBL kwa mara ya kwanza imetengeneza faida ya shilingi Million 318, kutoka kwenye hasara ya shilingi Million 600 katika kipindi Cha mwaka 2020.


Meneja wa Benki hiyo Jofrey Ng'ura ameyasema hayo katika Semina iliyofanyika July 29, Mkoani Kilimanjaro iliyowakutanisha wadau wa Ushirika Ili kujadali namna ya kukuza mtaji wa kuanzisha Benki ya Taifa ya Ushirika.


Ng'ura amesema uwepo wa Benki ya Taifa ya Ushirika,itasaidia wanachama wa vyama vya ushirika ambao wengi wao ni wakulima kufikiwa  na huduma za kibenki kwani asilimia kubwa hawatumii huduma hiyo.



Marajisi msaidizi wa vyama vya ushirika Tanzania Bara, Collins Nyakunga amesema kutokana na vita vya Ukrane na Urusi vimechangia Bei ya Pembejeo kuwa juu, na kukwamisha Juhudi za uwazishwaji wa Benki ya Taifa ya Ushirika kwa Wakati.


Hata hivyo Mwezeshaji kutoka Tanesco Saccos Andrew Hilary, amewataka Viongozi na wanachama wa Vyama vya ushirika kununua hisa za Benki hiyo Ili kufikia lengo la Ukusanyaji wa Shiling Billion 15.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI