Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa leo Julai 08, 2022 ameongoza umati mkubwa wa wananchi wa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi kutazama Filamu ya The Royal Tour kwenye uwanja wa Wandorwa wilayani hapa.
Akizungumza katika tukio hilo, Mheshimiwa Majaliwa ameutaka uongozi wa wilaya hiyo kuibua vivutio vya utalii ili wilaya iweze kunufaika na idadi kubwa ya watalii wanaoingia nchini na hasa baada ya hamasa kubwa iliyochochewa na filamu ya The Royal Tour.
“Migodi ya madini mbalimbali inayotarajiwa kufunguliwa hapa hivi karibuni ni fursa ambayo wakazi wa Ruangwa mnapaswa kuichangamkia kwa kuwekeza katika miundombinu itakayowawezesha wageni watakaokuja kupata huduma muhimu ikiwemo malazi, chakula, usafiri na huduma za afya ili kujipatia fedha”
0 Comments