Na Gift Mongi_Moshi
Ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya sikukuu ya wafanyabiashara maarufu kama sabasaba mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi amekabidhi vyeti kwa vijana walioshishiki kongamano la kibiashara lililofanyika kata ya Uru Kusini.
Kongamano hilo limeandaliwa na diwani wa kata hiyo Wilhad Kitaly ambapo pia limewakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara na wadau mbalimbali huku wajasiriamali nao wakipewa kipaumbele.
Mbunge huyo akiwa katika chuo Cha VETA Mawela alisema kutokana na serikali kuona makundi hayo ya wanawake vijana na makundi maalumu kwa kipindi kirefu yanakosa mitaji katika kujiajiri na kuendesha shughuli zao ndipo ulipoanzishwa mkakati huo wa kutoa mikopo isiyo na riba hivyo kila mwenye sifa anaweza kunufaika.
Alioongeza kuwa ipo haja Sasa kwa makundi hayo ya vijana wanawake na wenzetu wenye ulemavu kuona umuhimu wa kuchangamkia fursa hizo za mikopo ili kuweza kujikwamua kiuchumi sambamba kufikia malengo ya serikali.
Naye diwani Uru Kusini, Wilhad Kitaly aliwashukuru wananchi, wajasiriamali na wafanyabiashara wote waliohudhuria kongamano kwa kushiriki kupata maarifa na elimu kuhusu fursa mbalimbali za biashara.
Pia amewataka vijana kutochagua kazi za kufanya na kujitahidi kubadili changamoto kuwa fursa ili kuweza kujipambanua zaidi katika kupambana na uhaba wa ajira
Kwa upande wake katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro Willy Machumu amewataka vijana kufanya kazi kwa kujituma sambamba na kuongeza ubunifu kwani hali halisi ya maisha siyo rahisi kama wanavyofikiria.
Machumu alitoa rai hiyo katika kongamano la wafanyabiashara na wajasiriamali lililoandaliwa na diwani wa Uru Kusini Wilhad Kitally,ikiwa ni maadhimisho ya sikukuu ya wafanyabiashara.
Alisema wafanyabaishara wengi waliofanikiwa imetokana na jitihada binafsi katika kujituma lakini pia kuwa na malengo ambayo yanatekelezeka hivyo kuwa nyenzo muhimu katika kuyafikia mafanikio.
0 Comments