*********
Na Gabriel Kilamlya NJOMBE
Baadhi ya Wazee wa kijiji cha utengule kilichopoa kata ya utengule halmashauri ya mji wa Makambako wamemuomba Mbunge wa jimbo la hilo Deo Sanga kumuandaa mtu ambaye atampokea nafasi hiyo pindi atakapostafu.
Wakizungumza katika Mkutano wa Mbunge huyo kijijini hapo, Wazee hao wamesema kuna kila sababu ya Mbunge huyo kuandaa mrithi wake kwani bila kufanya hivyo jimbo hilo halitafanikiwa hasa kwenye utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo.
Wananchi hao wamesema Mbunge Deo Sanga amekua akijilotea fedha nyingi kupitia kampuni yake ya Jahpeople na kufanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali katika sekta ya afya, elimu na kusaidia wananchi wenye changamoto mbalimbali.
Jumla ya Vyumba vya madarasa tisa vinajengwa katika mitaa mbalimbali mjini Makambako mwaka huu kwa ufadhali wa kampuni ya JahPeople.







0 Comments