Na Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam
Taasisi ya Diamonds In the Sky Foundation leo imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye Thamani ya zaidi shill mill 4 kwa wanafunzi wenye uhitaji maalum katika shule ya msingi Yombo Dovya Temeke jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa utoaji wa vifaa hivyo vya msaada, Mbunge wa Jimbo la Temeke Dorothy Kilave amesema kitendo kilichofanywa na cha Taasisi hiyo ya Vijana wanaosoma nje ya nchi ni jambo la kupongezwa na kuungwa na mkono na jamii kwani watoto wenye uhitaji wapo wengi na baadhi yao hawajafikiwa.
Aidha, amewataka wadau wengine kujitokeza kwa wingi kuwasaidia watoto hao wenye uhitaji kwa kuwapatia vitu mbalimbali kama sehemu ya kuwatia moyo katika shughuli zao wanazofanya, huku akiwasihi wazazi na walezi kutowaficha watoto wao wenye ulemavu katika jamii waweze kufikiwa na misaada kiurahisi.
"Ninawaomba wazazi hasa kipindi hichi ambacho tunaelekea katika sensa ya watu na makazi kutowaficha watoto wao wenye uhitaji Ili na wao wewe ni sehemu ya watanzania watakaohesabiwa kwa ajili ya kupanga maendeleo ya Taifa"amesema Mbunge Kilave.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Jacqueline Lussa amesema wameamua kutoa msaada huo Ili kutoa hamasa kwa watu wengine ambao waweze kuiga mfano huo na kuweza kuwasaidia, ambapo Serikali imetenga mazingira mazuri kwa ajili ya watu wenye ulemavu ikiwemo kujenga vituo.
Aidha, amesema kuwa lengo la Taasisi hiyo ni kuhamasisha jamii juu ya kuwasaidia watu wenye uhitaji maalum kwa kuwapatia misaada mbalimbali, huku akiwataka wazazi na walezi kuwafichua waweze kuhesabiwa katika sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika August 23, mwaka huu.
Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Sondole Bulenga amesema Taasisi hiyo itaendelea kuwasaidia watoto wenye uhitaji maalum na kuongeza kuwa jamii ya Tanzania inapaswa kuondoa dhana ya kuwaficha watoto wenye ulemavu kwani wanawakosesha haki zao za msingi.
0 Comments