Header Ads Widget

WATU 8 WAFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI KAGERA HUKU WATANO WAKIWA NIWA FAMILIA MOJA.

 


NA, TITUS MWOMBEKI, KAGERA Matukio Daima App Kagera.


Watu wa nane  wamefariki  dunia kwa ajali ya gari  mkoani Kagera  baada ya gari  aina ya roli lenye namba ya usajili RFA 129W iliyokuwa na treila lenye namba RL 4367 aina ya Mercedes  Benz  kugongana uso kwa uso na gari namba T. 626 DRX aina ya TOYOTA SUCCED katika maeneo ya Busiri barabara kuu ya kutoka Lusahunga kuelekea wilaya ya Bihalamulo., tukio lililotokea Julai 11 mwaka huu.


Gari  aina ya roli lenye namba ya usajili RFA 129W iliyokuwa na treila lenye namba RL 4367 aina ya Mercedes  Benz  lilikuwa likiendeshwa na Vicent S/Ogakuba mwenye (52) Mnyarwanda mkazi wa Nyamata Rugesela East Provience-Rwanda kutokea Rwanda Kuelekea Dar Es  Salaam na gari namba T. 626 DRX aina ya TOYOTA SUCCED lilikuwa likiendeshwa na Nyakwenda S/O Bihela  (35) mkazi wa kijiji cha Kikoma, kata ya Lusahunga wilaya ya Biharamulo akitokea Nyamalagala kuelekea Benako wilaya ya Ngara.



Taarifa hiyo imetolewa na kamanda wa polisi mkoani Kagera,  Willium .T. Mwampaghale- ACP wakati alizungumza na waandishii wa habari ofisini kwake  ambapo amesema kuwa uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi umebaini chanzo cha ajari hiyo ni uzembe wa dreva wa gari namba RAF 129W baada ya kuhama kutoka upande wa kushoto kunda upande wa kulia.


“Ajali hiyo imesababisha vifo vya watu nane ambao ni dereva na mmiliki wa TOYOTA SUCCED na abilia wake saba waliokuwepo kwenye gari hilo, watu watano miongoni mwa hao waliopata ajali ni wafamilia moja kwa maana ya mama na watoto wake wanne”


“Nyawenda Bihela (35), Jesca Leonard (45),  Magreth Sekanabo (14), Adidas Sekanabo (12), Zabron Sekanabo(6), Vestina Sekanabo,(8) Michael Charles (28) na Majaliwa Manundo (32) na miili ya marehemu imeifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika kituo cha afya Nyakanazi”



Ameongeza kuwa mtuhimiwa Vicent A/O Gakuba ambaye ni dreva wa wa gari namba T.129W MERCEDES BENZ alijaribu kutoroka mara baada ya ajali hiyo lakini jeshi la polisi lilifanikiwa kumkamata  tarehe 11 nwezi July mwaka huu majira ya saa nne asubuhi akiwa ndani ya roli lililokuwa likielekea nchini Rwanda  akikwepa kukamatwa, na kuongeza kuwa mtuhumia huyo atafikishwa mahakamani mara baada ya taratibu za kiupelelezi kukamilika.


Kamanda Mwampaghale- ACP ametoa onyo kwa madereva wazembe wasiofuata sheria za barabarani kubadilika mara moja na kufuata sheria za barabarani kwani jeshi la polisi mkoani Kagera halitasita kumchukulia hatua kali dereva atakayebainika kutotii sheria za barabarani.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI