Header Ads Widget

WAUMINI WA KIISLAMU WATAKIWA KUFATA TARATIBU NA SHERIA ZA DINI

NA CHAUSIKU SAID,MATUKIO DAIMAAPP, MWANZA

Waislamu Mkoa wa Mwanza wametakiwa kufunga ndoa kwa mjibu wa sheria taratibu na misingi ya dini hiyo  ili kuepuka mauaji ya kindoa yanayoendelea katika jamii.

Hayo yamebainishwa na sheikh Mkuu wa Mwanza Hassan Kabeke na kusema kuwa inawezekana mauaji hayo yanasababishwa na mfumo holela unaotumika katika maisha.


Kabeke amesema kuwa kutokana na wanandoa kuingia kwenye ndoa kiholela  ndio maana mauaji ya wanandoa yanazidi kuongezeka hali ambayo inahatalisha usalama wa maisha yao

"Mfumo holela ni mtindo ambao mtu anaolewa au kuoa hapati mafunzo ya ndoa wakati dini yetu inatoa mafunzo hayo" Alisema Kabeke.

Hata hivyo amewataka waislamu wanapo wote wanapotaka kuingia kwenye ndoa lazima wapate mafunzo kuanzia wiki 14 hadi 21 yatayowasaidia kuishi katika ndoa kwa amani.


" Ni lazima kupata mafunzo hayo yatakayowasaidia kuishi kwa upendo na amani kwenye familia na kumuogopa Mungu kwa kufata mafundisho yake " Alisema Kabeke.

Kwa upande mwingine sheikhe Kabeke ameitaka serikali na wiazara ya mambo ya ndani kuhakikisha wanasimamia swala la vyeti vya ndoa kutokana na baadhi ya watumishi wa dini ya kiislamu wanapohitaji uahamisho, kupandishwa cheo,  pamoja na kukata bima ya afya wakiombwa vyeti vya ndoa ya serikali na cha dini hakitambuliki.

" kuna shida kubwa kwa waislamu hususani kwa wanaofanya kazi serikalini na mashirika imefikia hatua mtu anapohitaji kufanya jambo anapeleka cheti cha ndoa ya kiislamu haikitambuliki cha serikali ndio kinatambulika" Alisema kabeke.

Hata hivyo amesema kuwa serikali inaumuhimu wa kuangalia jambo hilo kwani linawapa shida waumini wa dhehebu hilo hususani wanapokuwa na mhitaji muhimu yanayohitaji cheti cha ndoa.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI