.
Bi.Rose Lisulile - Mwenyekiti wa kikundi cha RODAPEA.Na Frederick Siwale- Matukio daima media Njombe.
WATANZANIA umefika wakati wa kuacha kasumba ya kupenda "kasumba" ya kushabikia bidhaa za kigeni ili hali mali ghafi tunazo za kutosha hapa Nchini.
Rai hiyo imetolewa na Bi.Rose Lisulile, Mwenyekiti wa kikundi cha Wajasilia mali kilichopo mtaa wa Uzunguni kata ya Maguvani katika Halmashauri ya Mji Makambako Mkoani Njombe wakati akizungumza na Mwandishi wa Matukio daima media.
Alisema kikundi hicho kinafanyakazi ya kusindika vyakula na Wine kwa kutumia matunda ya asili aina ya msasati ,ufudu na mengineyo yanayoliwa na binadamu yale yanayolimwa kama nyanya na karoti.
"Watanzania tatizo letu ni kuendelea kuendekeza kasumba za kigeni na kuzifurahia kwa kupenda bidhaa zinazo zalishwa nje ya Nchi kwa kuamini kuwa ni bora na nzuri kuliko za kwetu kitu ambacho siyo kweli" Alisema Bi.Lisulile.
Alisema kikundi hicho cha RODAPEA pamoja na kuendesha shughuli za usindikaji wa vyakula na vinywaji kinajishughulisha pia na kilimo ili kuweza kupata mali ghafi za kuingiza kiwandani.
"Mwandishi wa habari niwashukuru sana Shirika la viwanda vidogo Nchini SIDO kwa kuniwezesha kupata mafunzo ya usindikaji na pia MVIWATA kunipatia mafunzo ya kilimo na kunipelekea kupata uwezo wa kuunda kikundi hiki cha RODAPEA.Alisema Bi.Lisulile.
Alisema changamoto ni sehemu ya mafanikio muhimu kuzidi kuboresha viwango bidhaa zetu ambazo mali ghafi zake zinapatikana hapa Nchini ambazo ni za asili tofauti na zile za Kigeni.
Upande wake mwanakikundi mwingine Bw.Edbon Mgimba kutoka Wilayani Ludewa alisema anashukuru sana Uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheli (KKKT) Ludewa kwa kuwaunganisha na RODAPEA na kupata elimu na ujuzi wa usindikaji.
Bw.Mgimba alisema kufuatia kupata ujuzi huo wito wake kwa Vijana wajikite katika uwajibikaji kwa kufanyakazi za kujiajiri badala ya kutegemea kupata ajira kutoka Serikalini.
"Vijana tusiendekeze vitendo vya uhalifu vya kuuza na kutumia dawa za kulevya au kufanya uporaji ili hali nguvu na akili hiyo tunaweza kuitumia kwa shughuli za uzalishaji mali na kujiinua kiuchumi." Alisema Bw.Mgimba.
Aidha Bi.Pelesi Kabehe mmoja wa wanakikundi hicho alisema anamshukuru sana Mwenyekiti wa RODAPEA kwa kumshirikisha katika shughuli hizo za usindikaji wa vyakula na vinywaji.
"Mimi nipende kutoa wito kwa akina dada wenzangu tusipende kujiingiza katika shughuli za kikahaba na ukiruka njia eti kwa lengo la kujikwamua kiuchumi ili hali shughuli za ujasilia mali zinaweza kutukwamua kiuchumi na kimaendeleo binafsi na kwa Taifa." Alisema Bi.Kabehe.
Hata hivyo kikundi hicho cha RODAPEA kimejipanga kushiriki Maonyesho ya nane nane ya Jonh Mwakangale kanda ya nyanda za juu kusini ili kupeleka bidhaa zake kule kwa ajili ya kutangaza soko.
Bi.Rose Lisulile - Akifunga kifungashio mtamboni.









0 Comments