Na Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam
Katika kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, chama waigizaji Tanzania (TDFAA) Mkoa wa Dar es Salaam Julai 30 wanatarajia kufanya utalii wa ndani katika Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi kwa lengo la kutangaza vivutio.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa TDFAA Leonard Piere Mwinuka amesema lengo la ziara hiyo ni kutangaza vivutio vya Utalii vilivyopo katika Wilaya hiyo ikiwemo misikiti 99 yenye majina ya Mwenyezi Mungu, magofu pamoja na kuona namna walivuotengeneza not yao wenyewe.
"Watu wengi wanajua vivutio vilivyopo Serengeti, mikumi lakini wamesahau kuwa pia kilwa kuna vivutio vyengine, tunapaswa kuwahamasisha Ili waende huko wakajionee na kufanya Utalii wa ndani"amesema Piere.
Kwa upande wake, Rais wa chama cha wataalamu wa figo ambaye pia ni Daktari Bingwa wa kwanza Nchini Tanzania kutoka Hospital ya Taifa ya Muhimbili, Dk Onesmo Kisanga amesema nijuhudi muhimu ya kuimarisha utalii wa ndani wao kama wataalamu wa figo wanawaunga mkono waigizaji .
"Wasanii ni watu ambao wapo karibu sana na jamii hivyo itasaidia kuongeza watalii wandani na tutawatumia kutoa elimu ya figo kulingana na utafiti tulioufanya 2014 kaskazini mashariki mwa Tanzania imebainika 6.7% ya wananchi wana wanasumbuliwa na marazi ya figo"amesema Dk Kisanga.
Mwenyekiti wa Sauti ya Mama ambae pia ni Muigizaji wa bongo movie Shamira maarufu kama Bi Staa amesema sasa ni zamu ya kilwa kutangaza vivutio kwa ajili ya kuvutia waekezaji kama anavyofanya Rais Samia kupitia filamu ya Royal Tour.
"Sisi kama waigizaji tumeungana kwa pamoja kumuunga mkono tunaenda kifua mbele kumwambia Mama asante kwakujua kazi yetu sio ya ubabaishaji kwa sapoti aliyotuonyesha kuwa sanaa ni kazi na sisi pia tunamuonyesha kuwa tuna uhuru wa kufanya kazi yetu "amesema Bi Staa.
Naye, Afisa utalii kutoka mamlaka ya usimamizi wa wanyama pori Tanzania (TAWA)Rweja Lugendo wameungana na waigizaji wa mkoa wa Dar es Salaam kutangaza utalii wa ndani amvao unajenga uchumi ambapo inaongeza kipato cha Nchi .
"Sisi TAWA tupo pamoja nao na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan baada ya kutangaza utalii nje na ndani kumekuwa na mwamko mkubwa sana wa wananchi kutembelea vivutio ,watatembelea Kilwa kisiwani na songo mnara"amesema Lugendo.






0 Comments