Header Ads Widget

WATAKIWA KUMALIZA MIRADI YA MAENDELEO KWA WAKATI.

 


Na Jusline Marco;Arusha


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella amewagiza viongozi wa Wilaya na Halmashauri hiyo kuhakikisha wanasimami miradi ya maendeleo ili iweze kukamilika kwa wakati na wananchi waanze kupata huduma.


Mongella ametoa maagizo hayo wakatika akiwa katika  ziara yake ya siku moja ya kukagua miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Karatu.



Katika ziara yake Mhe.Mongella amesisitiza kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kwa wakati kutasaidia kuongeza thamani ya miradi hiyo.


Aidha katika  mradi wa Kilimo cha Vitunguu katika Kata ya Mang'ola, Mongella amewaahidi wakulima hao kuwa atawasaidia kuwatafutia masoko ya vitunguu ya uhakika ili kilimo hicho kiweze kuwa na tija na manufaa kwa wakulima wenyewe na Taifa kwa ujumla.



Vilevile ameongeza kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo ili wananchi waweze kupata huduma bora na kwa ukaribi zaidi ambapo amewataka wananchi kuithamini na kuitunza miradi hiyo kwani ni kwaajili ya yao ili waweze kupata huduma muhimu kwa ukaribu zaidi.


Kwa upande wake  Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe. Dadi Holace Kolimba amesema wao kama Wilaya wanashirikiania kwa ukaribu sana na viongozi wa Halmashauri ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa haraka kama ilivyopangwa.


Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu  Karia Rajabu amesema watayasimamia maelekezo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa ili Halmashauri hiyo iweze kukamilisha miradi yote ya maendeleo kwa wakati.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS