Header Ads Widget

WALIMU SHULE ZA JUMUIYA YA WAZAZI CCM MARUFUKU KUJIHUSISHA NA SIASA.



Na Hamida Ramadhan Matukio Daima App Dodoma


MWENYEKITI wa  Jumuiya ya Wazazi wa  Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt, Edmund Mndolwa amewataka watumishi katika taasisi za elimu zinazomilikiwa na chama hicho kuacha kujihusisha na masuala ya siasa na badala yake kujikita zaidi katika  utoaji wa elimu iliyo Bora .



Mwenyekiti huyo aliyasema hayo leo Juni 15,2022 jijini Dodoma katika kikao cha Wakuu wa shule za Umoja wa Wazazi Tanzania .


Alisema kiwango cha ufaulu katika shule zinazomilikiwa na Chama zimeendelea kuonekana kuimarika siku hadi siku kwani hakuna shule yoyote iliyopata daraja sifuri


"Tunajivunia uwepo wa shule zetu hizi katika Jumuiya zetu kwani zimeweza kututoa kimasomaso katika matokeo ya  kidato cha Sita ninafuraha Kusema katika Shule zetu hakuna daraja 0 Wala  daraja la 4 haya ni mafanikio makubwa kwetu sisi kama Jumuiya," alisema Dkt,Mndolwa


Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa  Chama cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo akifungua kikaoo hicho alitoa wito kwa jumuiya ya wazazi wa chama hicho  kuendelea kuwajengea uwezo viongozi wa shule ili heshima ya wakuu wa shule iendane na muda aliokaa katika shule.



"Mpango wa chama hichi ni kuongeza tija katika kujenga mafanikio kwenye shule zinazomilikiwa na chama chetu," .


Na kuongeza "Lengo  la chama  kuanzisha shule ni kuwawezesha vijana wote kupata elimu iliyobora ambapo katika matokeo ya mtihani mwaka huu karibu asilimia 80 hadi 90 ya wanafunzi wanaosoma katika shule zinazomilikiwa na chama wamepata ufaulu wa daraja la kwanza na la pili huku mwanafunzi mmoja tu akipata ufaulu wa daraja la nne na nimepata taarifa hapa kulikuwa na changamoto kwa Upande wa mtoto huyo",alisema Chongolo



Aidha amewataka kwa wakuu wa shule kuendelea kujenga nidhamu katika shule wanazoziongoza katika kuendelea kujenga heshima ya chama.


"Heshima ya mwalimu ni matokeo bora hivyo niwatake kuwa awamu ijayo watatoa zawadi kulingana na kiwango cha ufaulu katika shule husika na kuwataka walimu kukaza buti katika ufundishaji.


 Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI