Na Amon Mtega, Mbinga
KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Jacob Siayi amesema takribani wanachama wapatao 400 wamechukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho wilayani humo, ameweka bayana siri ya wingi huo ni Imani na uzingatiwaji wa demokrasia ndani ya CCM.
"Idadi hii inatokana na mseto wa mambo mengi, mosi, upanukaji, ukuaji na uzingatiwaji wa demokrasia, Kwa maana ya usawa ndani ya CCM.
"Lakini pili, sisi viongozi wilayani tulifanya kazi kubwa ya kuhamasisha Kwa jitihada kubwa, watu kujitoa katika kuwania nafasi za uongozi, katika kada nyanja na ngazi mbalimbali," amesema na kuongeza;
"Tuliwataka pia viongozi wa maeneo husika kukaa ofisini na kuwahudumia watia nia wote wanaokuja kuchukua na kurejesha fomu hizo," amesema Siayi.
0 Comments