Mtendaj wa kata ya Butimba jijini Mwanza bw David Kyarwenda pamoja na mwenyekiti mtaa wa Mahina bi Mery Sule washutumiwa kuongoza wa vurugu za mgogoro wa ardhi katika eneo la kambarage, baina ya wananchi na mfanyabiashara maarufu Alhaj Yusuph Salehe Banyanga.
Akiongea na waandishi wa habari Alhaj Yusuph Banyanga amedai kuwa mnamo tarehe 3 july alipigiwa simu na mtendaji kuhuhudhuria mkutano na wananchi wa eneo hilo ili kubaini chanzo cha mgogoro uliopo. Lakin kwa mujibu wa Alhaji Yusuph Banyanga baada ya kufika eneo hilo la mkutano ambapo alikaribishwa na viongozi wa serikali , mwemyekiti, mtendaji pamoja na diwani , Yeye alijibu nanukuu" hata nishakaribia hata msingekaribisha".
Aidha baada ya kauli hiyo alishambuliwa na yeye na familia yake..
Mtendaji wa kata hiyo amekiri kutokea kwa vurugu hizo baina ya familia ya Banyanga na wananchi, na kusema kuwa wao kama viongozi walijitaidi kuzuia vurugu hizo, na kuwaahidi wananchi kuleta wataalamu wa ardhi ili kujiridhisha uhakika wa mipaka na umilik halali wa eneo husika linaloleta mgogoro.
Baadhi ya wananchi waliokuwepo eneo la tukio wamekiri kutokea kwa mgogoro huo na wamedai kua mwenyekiti wao mele sule ndie tatizo .
0 Comments