Header Ads Widget

MATATANI KWA KUFANYA VITENDO VTA USHIRIKINA KWENYE CHANZO CHA MAJI MYO NJORO


Na Gift Mongi,MatukioDaimaApp,

Moshi

Kwa kile kilichoonekana si Jambo la kawaida kujitokeza watu wawili wamekamatwa kwa kufanya vitendo vya kishirikina  kwenye chanzo cha maji mto Njoro huku wengine zaidi ya 10 wakichukuliwa hatua mbalimbali za kisheria baada ya kubainika kufanya uharibifu wa mazingira.


Matendo yalioonekana wazi kuwa na dalili za ushirikiana ni pamoja na waliovamia eneo la mita 60 katika vyanzo vya maji na kuwekewa mawe ya mipaka 'Bicons' katika makazi yao kutaka mamlaka zishindwe kuwahamishwe.


Habib Lema i mwenyekiti wa kamati ya watumia maji katika mto Rau, Habibu Lema alisema hayo wakati bodi ya Maji bonde la Pangani (PBWB),ikihamasisha jamii kusafisha mto huo kwa kuondoa taka na kurejesha kina halisi Cha mto huo.


Lema alisema June 30 mwaka huu majira ya saa 3.00 asubuhi watu wawili ambao ni wanawake wenye wastani wa umri wa miaka 50 na kuendelea  ambao pia majina yao yamehifadhiwa walikutwa wakifanya vitendo vya kishirikina katika mto huo.


"Tumewakuta wakimwagiana maji na kuimba nyimbo ambazo hazieleweki lakini pia tumekuwa tukichukua hatua kwa kutoza faini wanaotiririsha maji taka na uchafu mwingine ndani ya mto Rau na Njoro,"alisema Lema


Alisema kuwa wananchi wanaoishi katika eneo la mita 60 na kuwekewa 'beacons'ili wahame wamekuwa 

wanafanya ushirikina wakitaka PBWB pamoja na viongozi wa watumia maji na serikali washindwe kuwahamisha.


Mhandisi wa mazingira kutoka bonde  la Pangani(PBWB)aArafa Majid alisema kampeni ya kusafisha mito hiyo ni sehemu ya bonde kutimiza miaka 31 tangu kuanzishwa kwake.


Kwa mujibu wa mhandisi Arafa ni kuwa 

kampeni hiyo umefanyika pia katika mikoa mingine ya kanda ya Kaskazini inayopitiwa na bonde hilo lengo likiwa ni kutunza mazingira ya bonde hilo.


"Kampeni hii inahusisha utoaji wa elimu kwa wananchi kuheshimu eneo la mita 60, kutotiririsha maji machafu,utupaji wa taka na wananchi na viongozi kuondoa taka zinazopunguza kina Cha mto"alisema.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI