Header Ads Widget

UJENZI WA CHUO CHA UALIMU SUMBAWANGA WAFIKIA ASILIMIA 61.4 HADI SASA

NA FRANCO NKYANDWALE MATUKIO DAIMA APP SUMBAWANGA.

SHILINGI BIL.3,852,697,911 zinazotumika katika awamu ya kwanza ya kujenga majengo 11 ya chuo kipya cha Ualimu Sumbawanga eneo la Pito lilipo kwenye Halimashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ambapo mradi huo umefikia asilimia 61.4 hadi sasa.


Akizungumza leo kwenye ukaguzi wa mradi huo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti amewaleza waandishi wa habari kuwa serikali inatekeleza mradi huo kwa lengo la kufungua fursa za kielimu kwa wananchi ambapo utakapokamilika utasaidia kuchochea ukuaji wa uchumi na kuongeza wataalamu wa Elimu.


"Rukwa tumenufaika na mradi huu wenye thamani ya shilingi Bilioni 3.9 ambapo majengo kadhaa yamekamilika na mengine jitihada za ukamilishaji zinaendelea vizuri. Nimeridhishwa na  kazi inayoendelea hapa na kuhusu changamoto chache nitawasiliana na Wizara ya Elimu tuzitatue mapema na mradi ufikie mwisho" ,alisema Mkirikiti.


Akizungumzia utekelezaji wa mradi huo Mhandisi Mshauri toka Chuo cha Ufundi Arusha Emanuel Didas amesema mradi umefikia asilimia 61.4 za ujenzi ambapo jumla ya shilingi Bilioni 2.5 kati ya shilingi Bilioni 3.0 zilizopokelewa mwezi Mei mwaka huu zimetumika hadi sasa.



Mhandisi Didas amesema jumla ya majengo 11 yamejengwa na yapo katika hatua za ukamilishaji ikiwemo jengo la madarasa lenye vyumba 8, mabweni mawili yenye uwezo wa wanafunzi 250 kila moja, vyoo vya nje, nyumba za watumishi, jiko, bwalo na vibanda vya walinzi.


Mradi wa ujenzi wa chuo cha Ualimu Sumbawanga awamu ya kwanza kupitia mradi wa Education Program for Results (EP4R) chini ya Wizara ya Elimu ulianza 15 Agosti 2021 na unatarajiwa kukamilika mwaka huu Mhandisi akifafanua.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI