Header Ads Widget

BREAKING:DKT SHOO AFARIKI DUNIA

Mwandishi wa habari mkongwe nchini, Dk. Gideon Juma Safari Shoo, aliyefariki dunia jana, Jumamosi, Julai 9, 2022, akiwa na umri wa miaka 66, atazikwa Jumatano mchana, Julai 13, mwaka huu mjini Dar Es Salaam.

Msemaji wa familia ya Shoo, Bwana Kodi Siarra, amethibitisha leo, Jumapili, Julai 10 kuwa Dk. Shoo atazikwa katika Makaburi ya Kondo, Kunduch, Dar Es Salaam, mchana wa Jumatano.

Mazishi ya Dk. Shoo yatatanguliwa na shughuli ya kumwaga mwandishi wa habari huyo msomi na nguli, itakayofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.Dk. Shoo ni mwanzilishi na mwanahisa wa Shule hiyo.

Shughuli hiyo ya kumuaga Dk. Shoo itaanza saa tano asubuhi kufuatia siku nne za msiba unaoendelea nyumbani kwake, Salasala, mkabala na mitambo ya umeme ya IPTL.

Dk. Shoo aliaga dunia baada ya kupigania maisha yake kwa siku 16 katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) cha Hospitali ya Muhimbili Orthopaedic Institute (MIO) katika Hospitali Kuu ya Taifa ya Muhimbili, Dar Es Salaam.

Dk. Shoo alifikishwa Moi asubuhi ya Alhamisi, Juni 23, mwaka huu baada ya kupata shambulio kubwa la kiharusi cha kichwani (hemorrhage stroke) kilichopasua baadhi ya mishipa ya damu, na alipoteza fahamu akiwa njiani kupelekwa Muhimbili.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI