Afisa Usalama wa Shirika la Tanesco Mkoa wa Tanga Emanuel Kimario akizungumza na waandishi wa habari leo .
Na Oscar Assenga, Tanga 
SHIRIKA
 la Umeme nchini Tanesco limewaonya wananchi wenye tabia za kuhujumu 
miundombinu kuacha mara moja tabia hizo kabla hawajachukuliwa hatua kali
 za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani na kifungo. 
Onyo hilo
 lilitolewa na Afisa Usalama wa Shirika la Tanesco Mkoa wa Tanga Emanuel
 Kimario  wakati akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu 
changamoto zinazosababisha ukosefu wa umeme kutokana na uharibifu na 
hujuma kwenye miundombinu ya shirika hilo. 
Alisema vitendo hivyo
 vinafanywa na baadhi ya wananchi wasio waaminifu na kusababisha shirika
 kutumua fedha nyingi kurudisha huduma na shughuli za umeme katika hali 
ya kawaida na pia kupelekea wateja kukosa huduma hiyo na kuzorotesha 
shughuli za kiuchumi za kila siku. 
“Lakini kutokana na gharama 
kubwa ambazo zinatumika kurudisha huduma kutokana na uharibifu shirika 
linaingia gharama kubwa na hivyo kupunguza kasi ya usambazaji wa umeme 
kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa na umeme”alisema 
Hata hivyo 
aliomba wananchi wawape ushirikiano kwa kuwafuchua wananchi ambao 
wamekuwa wakihujumu miundombinu ya shirika hilo  ikiwemo kutoa taarifa 
kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili waweze kuchukuliwa hatua na 
kuhakikisha miundombinu yao inakuwa salama na huduma inapatikana 
ipasavyo. 
“Tumekuwa tukifanya operesheni kwa kushirikiana na 
vyombo vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha huduma inapatikana na pale 
ambapo mwananchi anabainika amehujumu miundombinu kunawachukuliwa 
hatua”Alisema 
Aidha alisema hivi karibu kwa kushirikiana na 
vyombo vya ulinzi na usalama kulitokea hujuma kwenye maeneo yao na 
walifanikiwa kuwamata baadhi ya watuhumiwa mashauri yao yapo mahakamani 
na mmoja wapo alifunguliwa shauri la uhujumu uchumi namba 1 la mwaka 
2022 na limemalizika na mtuhumiwa amehukumiwa kwenda Jela miaka 20. 
  
Alisema hatua ya kukamatwa mtuhumiwa huyo na wengine ambao mashauri saba yanaendelea kwenye mahakama za wilaya za Handeni,Lushoto na Tanga mjini ambapo kati ya hayo mawili yametolewa hukumu ni kutokana na operesheni ambayo wameifanya kushirikiana na vyombo vyengine vya usalama na kufanikiwa kuwakamataa.
Alimtaja 
mtuhumiwa huyo kuwa Mohamud  Hamisi shauri hilo lilimalizika Julai 12 
mwaka huu huku akitoa rai kwa wananchi kulinda miundombinu na kuitunza 
ikiwemo  kutambua kwamba ni jukumu  la watu wote kuilinda na wale 
wanaofanya hujuma kuacha kufanya hivyo  kwani hawapo tayari kuona watu 
wachache wanahujumu muindimbiu hiyo . 
Mwisho.





 
 
 
 
 
 
 
 
.jpg) 
0 Comments