Na Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam
Waziri wa katiba na Sheria Damas Ndumbaro anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa wadau ulioandaliwa na Wakala wa Usajili na Udhamini RITA ambao umelenga kujadili kwa pamoja walipotoka, walipo sasa na wanapotaka kwenda.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu RITA Angela Anatory amesema kuwa, mkutano huo, utatoka na maadhimio ya nini kifanyike katika utoaji wa huduma zao Ili kuboresha zaidi kuwafikia wananchi wengi zaidi.
Amesema kuwa, Katika Mkutano huo utahudhuriwa na viongozi wa Dini, Wizara mbalimbali, Taasisi za Serikali mabalozi mbalimbali pamoja na wadau wengine ambapo miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa ni pamoja na mafanikio walioyapata, Changamoto pamoja na kujiwekea mikakati ambayo itasaidia kuzitatua na kusonga mbele.
Aidha, amesema kuwa, katika eneo la utoaji wa huduma wamebuni program ya Usajili wa watoto chini ya umri wa miaka mitano ambapo imefanya vizuri kutoka asilimia 13 hadi kufikia asilimia 65 katika mikoa 23 ya Tanzania Bara ambapo watoto mill 7.7 wameshasajiliwa.
Hata hivyo, ametoa rai kwa wananchi kuendelea kutumia huduma mbalimbali zinazotolewa na Rita ikiwemo kufilisi na kudhamini, kusajili Talaka, ndoa, vyeti vya vizazi na vifo, kusimamia mali ambazo hazina mwenyewe, na za watoto ambao hawajafikisha miaka 18, kusajili mirathi, kuwasili watoto pamoja na kuandika wosia.
"Kumekua na changamoto nyingi za watu kutopata mali zao baada ya watu wanapoachana ama kufariki, ndio maana tunataka tukae pamoja tujadili namna bora ya kuweza kutatua changamoto hizi, tunafanyakazi kwa kushirikiana na watu wa Ustawi wa Jamii tupo nao karibu kuhakikisha mambo yote yanakwenda vizuri"amesema Angela.
Ameongeza kuwa, pia wamekua wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo wananchi kutokua na elimu ya kutosha juu ya huduma zinazotolewa na Wakala huo pamoja na kutokua na rasilimali watu wa kutosha kwa ajili ya kutunza kazi data na kutunza taarifa.
0 Comments