Header Ads Widget

SOKO LA PARACHICHI LADORORA.

 


Na Gabriel Kilamlya NJOMBE


Msimu ujao wa kilimo umeripotiwa huenda ukasababisha maafa makubwa kwa wakulima katika soko la zao la Parachichi endapo hatua za utafutaji masoko ya uhakika hazitochukuliwa mapema kwani   wengi wamewekeza mabilioni ya fedha kwenye kilimo hicho mkoani Njombe.


Hatua hii inakuja kufuata kuwapo kwa mdororo mkubwa wa soko la Parachichi katika msimu huu kwa wakulima wengi uliosababisha matunda mengi kuozea shambani na kusababisha hasara kubwa ikiwa vita vya Ukraine na Urusi vikitajwa kuwa sababu kubwa.



Kwa kuliona hilo Asasi isiyo ya kiserikali ya kilimo  mkoani Njombe ya NSHDA   chini ya mkurugenzi wake Frank Msigwa imelazimika kuanza kutafuta masoko katika mataifa mbalimbali ambapo Safari hii imelileta kampuni kubwa la Agromovil  toka nchini Marekani ili kujadiliana na wakulima namna ya kuliendea soko katika msimu ujao wa kilimo.


Maofisa toka taasisi ya kilimo Cha matunda na mbogamboga TAHA wamesema wanaowashawishi wakulima kuachana na kilimo cha parachichi wanapaswa kupuuzwa na kupingwa vikali mchana kweupe.


Kwa upande wake mteknolojia wa kampuni ya Agromovil ya nchini marekani inayofanyakazi ya kuwaunganisha wakulima na wanunuzi bwana Jan Fransis amesema kuwa ujio wao nchini ni kutaka kuwasaidia wakulima wa Parachichi hususani wa mkoani Njombe ili waweze kukutanishwa na wanunuzi hao.



Baadhi ya wakulima wa parachichi toka mikoa mbalimbali nchini pamoja na wadau wa kilimo akiwemo Leonard Mhidimba,Hombe Kaduma na Bokela Mwakabango ambaye ni mkuu wa Masoko na mauzo toka kampuni ya Sim solar inayosaidia wakulima kupata huduma ya maji ya umwagiliaji kwenye mashamba yao wanakiri kuanza kupata mwanga katika kilimo cha parachichi ambacho baadhi ya raia wamekuwa wakiwakatisha tamaa.


Kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe afisa biashara  mkoa wa Njombe Lusungu Mbede anasema serikali itaendelea kuwa bega kwa bega na wakulima katika kuhakikisha kilimo kinawasaidia kujikwamua kiuchumi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI