Header Ads Widget

SIKU YA MKULIMA WA PAMBA PAMBA IGUNGA

 


Na junior Mwemezi Igunga Tabora 


Wananchi mkoani tabora wameshiriki siku ya mkulima (Farmer Field Day) ambayo  imefanyika katika kijiji cha Bwabakima kata ya  Mbutu na Wilaya ya Igunga- Tabora 


Mgeni rasim katika siku   Mkuu wa Wilaya ya Igunga ambaye kutikana na majukumu mengine  aliwakilishwa na Bi. Martha Teveli amewataka wakulima wa pamba katika wilaya ya Igunga kulima kilimo chenye tija na kufata ushauri  wa wataalam wa kilimo kutoka Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania  TARI


Siku hiyo imeudhuriwa na baadhi ya viongozi ambao ni pamoja  mwakilishi wa ubalozi wa Brazil, Bodi ya pamba,  mwakilishi wa Wizara ya Kilimo, wawakilishi wa uongozi wa Mkoa Tabora na wilaya Igunga, Wakulima hodari na Maafisa Ugani wa wilaya zote za Tabora, watafiti toka Makao Makuu Dodoma na TARI Ukiriguru -Mwanza. 



 Mradi wa Cotton Victoria  ni matokeo ya ushirikiano wa Serikali ya Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania na Brazil katika kumsaidia mkulima  kuzalisha zao la pamba kwa tija. Mradui huu ulianza mwaka 2017 kwa mikoa ya Mwanza, Geita, Simiyu,  Shinyanga,  Mara na sasa Tabora na Katavi. 


Matokeo ya utafiti yamebainisha kuwa pamba ikipandwa kwa nafasi ya sentimita 60 kwa 30 (mbegu mbili kwa shimo) huwa na idadi ya 


mimea 44,444 mara mbili ya aliyepanda kwa nafasi ya zamani ya sentimita 90 kwa 40 (mbegu mbili kwa shimo) ambayo huwa na idadi ya mimea 22,222 kwa eneo hilohilo.


 Tija imeonekana kuwa kubwa kwa mkulima aliyepanda kwa nafasi ya sentimita  60 kwa 30 akifanikiwa kutunza vitumba 10 tu kwa kila mmea kwani ana uhakika wa kuvuna wastani wa kilo 700 hadi 1,400  kwa ekari (yasni kilo 2,000 hadi 3,000 kwa hekta)  huku akiwa amefuata kanuni bora za kilimo cha pamba. Ukilinganisha na aliyepanda kwa sentimita  90 kwa 40 mavuno ni wastani wa  kilo 200 hadi 300  kwa ekari.


 Changamoto kubwa kwa wakulima wengi imeonekana ni kuchanganya pamba na nazao mengine na kutozingatia kanuni bora za kilimo cha pamba. 



Hivyo, elimu ya  upandaji kwa nafasi mpya na matumizi ya kanuni bora za kilimo cha pamba yamesisitizwa kwa wakulima hodari na maafisa ugani wa wilaya za mkoa wa Tabora walioshiriki   mafunzo na Siku ya Mkulima kuwa mabalozi wazuri katika kusambaza teknolojia hii kwa wakulima wengine katika maeneo yao.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI