Header Ads Widget

SHEIKHE MUSTAPH AWAHIMIZA WAISLAM KUSHIRIKI KIKAMILIFU ZOEZI LA SENSA.



Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


SHEIKHE Mustaph Rajabu, amesema zoezi la sensa ya Watu na makazi linalotarajiwa kufanyika mwezi ujao ni jambo muhimu kwa waislamu kushiriki ili kuiwezesha serikali kupata takwimu sahihi zitazoisadia kuhudumia wananchi wake kwa mujibu wa idadi yao bila kumwacha hata mmoja


Rai hiyo ilitolewa leo na Sheikhe wa mkoa wa Dodoma Mustapha Rajabu, alipokuwa akizungumza na waumi wa dini hiyo kwenye ibada ya sikuku ya Iddi El Haji iliyofanyika kwenye msikiti wa Gadafi jijini Dodoma.


Sensa ya Watu na Makazi inayotarajia kufanyika mwezi ujao, ili kuiwezesha serikali kupata takwimu sahihi zitakazotumika kupanga mipango ya maendeleo kulingana na idadi halisi ya Watanzani.


“Mwaka huu taifa letu linakwenda kutekeleza zoezi muhimnu sana la sensa ya watu na makazi hivyo ndugu zangu waislamu nawaombeni sana kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hili ili kuiwezesha serikali yetu kupanga mipango kutokana na idadi yetu.


“Sensa ni agizo hata katika vitabu vya dini zetu hivyo wajibu wa kila mmoja wetu kujitokeza kuhesabiwa ili viongozi wetu watuhudumie kulingana na idadi yetu kwani sensa itaiwezesha serikali kujua wagonjwa wangapi,walemavu wangapi,wajane wangapi maskini wangapi ili iweze kutuhumia mahitaji yetu kulingana na idadi yetu vinginevyo itakuwa ngumu kutufikia wote bila kujua tuko wangapi”alisisitiza Shekhe Rajabu


Hata hivyo aliwataka waislamu kuendelea kuliombea taifa pamoja na viongozi wake ili kuwatumikia wananchi wake.


Kwa Upande wake Katibu wa msikiti wa Nunge jijini hapa Yahya Kivuma, akitoa mawaidha katika ibada ya Iddi iliyofanyika kwenye uwanja wa Jamuhuri aliwataka waisalamu wenye uwezo kuwasaidia wenye uhitaji.


Kivuma, alisema ni jambo lisilompendeza Mungu kwa watu wenye uwezo kutowasaidia wenye uhitaji na kuwaacha waendelee kuomba mitaani.


“Wapo waislamu wenzetu leo hii ni maskini lakini wale wenye uwezo hakuna hata mmoja ambaye anaweza kuwasaidia kuna watu wagonjwa, yatima, wajane lakini pia wapo ambao wanaihitaji mitaji ili kujikwamua kiuchumni lakini waislamu tunashindwa kuwasaidia hii ni sawa na kuwaibia”alisema


Hata hivyo, aliwataka waislamu wenye uwezo kifedha kusadia mambo yanayohusu dini badala ya kuendelea kusaidia michezo na ngoma.


“Hapa Dodoma kuna waislamu matajiri zaidi ya 100 lakini wanaosaidia mambo ya mungu hawazidi watano kwenye michezo tunawaona lakini ukiwambia hata kusaidia msikiti hawataki tubadilike ili tumutumikie Mungu kwani mali hizo ipo siku atazichukua na wewe utarudi huku kwa wasio kuwa nacho”alisema


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI