Header Ads Widget

RIDHIWAN KIKWETE APONGEZA MRADI WA VIWANJA 1,061 IRINGA ATAKA MIKOA MINGINE KUFIKA KUFIFUNZA ,AZUIA MAKABURI KUHAMISHWA

 

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete akitazama ramani ya viwanja vipya 1,061 eneo la Mgongo Manispaa ya Iringa jana .

NAIBU  waziri  wa Ardhi ,Nyumba na maendeleo ya Makazi  Ridhiwan Kikwete amepongeza  mradi  wa upimaji  viwanja  1,061 vya Mgongo katika   Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa na kuagiza eneo  lenye makaburi ya  wananchi  kuacha wazi  ili  kuepuka kurejesha machungu kwa  ndugu   wakati wa kuhamisha upya makaburi hayo .Mwandishi Francis Godwin MatukioDaimaAPP,Iringa


Akizungumza jana baada ya kutembelea eneo hilo la viwanja vya Mgongo vilivyopo nje kidogo na Manispaa ya Iringa , Kikwete alisema Kuna haja ya mikoa mingine kufika kujifunza Iringa jinsi ya matumizi mazuri ya Ardhi na mpangilio mzuri wa viwanja hivyo .

Huku akisisitiza maeneo hayo yenye Makaburi ya wananchi kuachwa bila  wazi badala ya kupima na kulipa fidia wananchi ,kwani Kwa kufanya hivyo kutapunguza malalamiko ya wananchi na kuepusha machungu ya kuzika upya mabaki ya miili ya marehemu hao .

"Niombe Sana maeneo ya maziko ya wananchi kutoyagusa kabisa kuacha kama yalivyo maana kuchukua maeneo haya itapelekea kurejesha upya vilio Kwa raia "

Katika hatua nyingine Kikwete aliagiza wananchi wote walionunua viwanja eneo hilo kuvilipia Kwa wakati ili Serikali kuendelea na huduma za kijamii na upimaji wa maeneo mengine .

Alisema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imedhamilia kuendelea kuboresha mazingira Bora Kwa wananchi na hivyo hakuna sababu ya wananchi kuendelea kujenga maeneo yasiyoruhusiwa na kuwa wale watakaovamia maeneo ya wazi hawatalipwa fidia na badala yake wataondolewa kupisha maeneo hayo .


Kwa upande wake kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Iringa  Fred Mgeni alisema eneo hilo la Viwanja vya Mgongo Lina jumla ya viwanja 1060 ambavyo tayari vimepimwa na eneo hilo lilikuwa Shamba la mwekezaji ambae alishindwa kuendeleza na Serikali ikamlipa fidia ili eneo hilo litumike Kwa Makazi ya wananchi .

Alisema kuwa Halmashauri ya manispaa ya Iringa ipo katika wilaya ya Iringa, mkoani Iringa. Manispaa hii ina
jumla ya kata 18 zenye mitaa ipatayo 192.

Kuwa  Halmashauri hii inapatikana katika latitude 7 kusini
mwa ikweta na longitude 34 mashariki ya greenwhich meridian, vile vile manispaa hii ina jumla
ya eneo lenye ukubwa wa kilometa za mraba zipatazo
Kwa mujibu wa mpango kabambe wa manispaa hii, manamo mwaka 2015, idadi ya wakazi
ilikua 283,580. Hadi kufikia mwaka 2021, idadi ya wakazi imefikia 311,916 kwa kiwango cha
ukuaji wa watu 1.6% kwa mwaka.

Uendelezaji wa mji katika maeneo mbalimbali unafanyika kwa kufuata mpango kabambe
(master plan) wa mwaka 2015-2035. Kwa kiasi fulani mpango huu umesaidia kutoa dira na
kudhibiti uendelezaji wa maeneo mbalimbali kwa mujibu wa sheria ya miongozo mbalimbali ya
ardhi. 
"Makazi yaliopangwa yamechukua kiasi takribani asilimia 47 ya eneo lote la manispaa.
Makazi yaliopangwa yamechukua kiasi cha asilimia 22 ya eneo lote la asilimia iliyobaki 31
inayojumuisha maeneo hatarishi, milima na mito/vijito ambavyo kwa sehemu kubwa yamebaki
kama yalivyo."

Mgeni alisema Sababu zilizosababisha kuhitaji mradi huu Mahitaji makubwa ya viwanja vilivyopimwa kutokana na kasi ya ukuaji wa manispaa ya
Iringa hususani mahitaji ya viwanja kwa ajili ya makazi, taasisi na uwekezaji wa
viwanda.

 Kuwepo kwa ujenzi holela kunakosababishwa na uhaba wa viwanja vilivopimwa,Kuwepo kwa uharibifu wa mazingira kunakosababishwa na ujenzi holela na shughuri
nyingine za binadamu,Kuchangia kufikia malengo ya mkoa wa Iringa ya kuandaa hatimiliki na makusanyo ya
kodi za ardhi,Kuongeza mapato ya serikali yanayotokana na mauzo ya viwanja na Kusogeza huduma za kijamii kwa ujumla kama vile barabara, maji na umeme.

Alitaja manufaa ya mradi
Mradi huo kuwa  utakua na faida kwa pande zote mbili yaani serikali na wananchi kwa ujumla.
Manufaa haya ni kama ifuatavyo:

 Ikiwa ni pamoja na Kuiingizia serikali mapato yanayotokana na uuzaji wa viwanda pamoja na kodi, Kuwezesha mji kupanuka kwa mpangilio mzuri kwa mujibu wa sheria, kanuni na
taratibu za ardhi na mapango kabambe uliopo Kupunguza uhaba wa viwanja vilivyopangwa kwa kupimwa na wananchi.


Aidha Kupata fedha za kuendeleza miradi mipya ya upimaji viwanja katika maeneo
mengine yanayokua kimji katika halmashauri zote za mkoa wa Iringa.

Eneo la mradi na idadi ya viwanja
Mradi huu wa kupanga, kupima na kumilikisha (kkk) katika eneo la mgongo
lililopo manispaa ya Iringa umetekelezwa na kusimamiwa na ofisi ya ardhi ya
mkoa kwa kutumia wataalamu wake wa ardhi waliopo na kampuni binafsi ya
upimaji. 


Eneo la mradi lipo upande wa kaskazini- magharibi mwa kitovu cha
manispaa umbali wa takribani kilometa 9. 

Aidha eneo lipo jirani kabisa (km3.5)
na barabara kuu ya Iringa-Dodoma na lina ukubwa wa ekari 576. Awali eneo hili
liikua likitumika kwa ajili ya shughuli za kilimo cha mazao mbalimbali kama vile
mahindi, alizeti, mbogamboga, maharage, nyanya 
Jumla ya viwanja 1,061 vimepangwa na kupimwa katika eneo hili kama Matumizi ya kiwanja Idadi Makazi (665),Makazi/ biashara (330),Shule ya awali (3),Shule ya msingi (2), Shule ya sekondari (1),Makazi mkusanyiko (1)Soko (2),Ibada( 3) Maziko (2) na zahanati (2)

Pia kutakuwa na mashamba mjini (26), stendi ya daladala (1) ,hoteli (2) na huduma nyingine nyingi 


Alisema Gharama za mradi huu jumla ya shilingi 449,844,000.00 zimetumika kwa ajili ya
ulipaji wa fidia ya ardhi na mali, upangaji na upimaji wa vipande vya ardhi, umilikishaji,
usimamizi na ufuatiliaji matangazo kwa njia ya redio na vipaza sauti barabarani pamoja
na kufungua barabara zenye urefu wa kilometa 30.5 ( shughuli hii bado inaendelea kwa
sasa). 

Kuwa fedha hizo ni sehemu ya mkopo wa shilingi milioni 450,000,000.00 zilizopatikana 
kutoka wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi.
Bei za viwanja na urejeshaji wa gharama za mradi
Urejeshwaji wa gharama za maradi utategemea mauzo yatokanayo na viwanja
vitakavyopimwa. Aidha bei ya viwanja inatarajiwa kuanzia shilingi 500-1500 kwa mita
moja ya mraba kutegemeana na matumizi ya kiwanja husika na ukanda uliopo.

Mapato kutokana na mauzo ya viwanja 1,036
Mapato kutokana na mauzo ya viwanja ni Tsh 1,701,800,000 wakati Mapato kutokana na kodi mbalimbali=154,954,260 na Jumla ya mapato yote 1,856,754,260 

Kwa upande wake mwenyekiti wa Mtaa wa Mkalagala Benjamin Ngailo alipongeza Serikali Kwa utaratibu huo na kuwa hakujawa na usumbufu wowote Kwa wananchi .


















Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI