Teddy Kilanga, Arusha
Naibu Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel amekemia tabia inayojitokeza sasa kwa baadhi ya watumishi wa serikali wanaokwamisha utoaji wa huduma za uchunguzi wa maradhi na tiba bure kwa Watanzania wenye uhitaji na wasiokuwa na uwezo.
Dkt.Mollel ametoa onyo hilo wakati anazindua kambi ya matibabu ya afya ya kinywa na meno bure inayotolewa na wataalamu kutoka taasisi ya Smile Star Care ya Nchini Uingereza na katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Arusha ya Mount Meru.
Aidha amesema hatua itakayofuata nikuwafurumua watumishi waliopo wizarani katika nafasi zao endapo wakiwa vikwazo kwa wadau wanaotoa huduma mbalimbali za afya kwa wahitaji.
"Serikali inasidiwa kupunguza gaharama ya kununua vifaa mbalimbali alafu unakuta mtu yupo amekaa huko wizarani na kuleta vikwazo wa vifaa hivyo kuingia nchini Tanzania kwani suala hilo hatutalivumilia na nikisikia mdau yoyote atakayeleta vifaa anacheleweshwa,"alisema Dkt.Mollel.
Kwa upande wake Kaimu Mganga mkuu wa mkoa wa Arusha,Dkt.Kipapi Mlambo alisema zaidi ya wagonjwa wa meno wameshapata huduma hiyo ikiwa wingi huo unaonyesha hali ya kukithiri kwa tatizo la meno kwa wananchi wengi.
"Tumekuwa na tatizo kubwa ya meno na kinywa wakati mwingine ni kwasababu ya uelewa hafifu au kutofikiwa na huduma na hata wengine kutokufika katika vituo vya afya kwa ajili ya kupatiwa huduma inayotakiwa,"amesema.
Kwa upande wake mbunge wa Arusha mjina Mrisho Gambo ameeleza huduma ya meno imekuwa msaada kwa idadi kubwa ya wananchi kutokana na uwezo duni
Naye Mdau wa sekta ya afya ambaye ni Mkurugenzi wa AVCO,Kake Dhariwal amesema katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma mbalimbali katika hispitali ya rufaa ya mountmeru anampango wa ujenzi wa jengo la wagonjwa Saratani.
Aliongeza kuwa lengo la ujenzi wa jengo hilo la Zahanati kuwapunguzia gharama wagonjwa wa saratani kufuata huduma hiyo nje ya mkoa.
0 Comments