Header Ads Widget

MBUNGE PROF. NDAKIDEMI ASHIRIKI ADHIMISHO LA MISA TAKATIFU SEMINARI YA MTAKATIFU JACOB.

 



NA WILLIUM PAUL, MOSHI.

Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini Prof. Patrick Ndakidemi ameshiriki katika adhimisho la Misa takatifu katika Seminari ya Mtakatifu Jacob (St James Seminary) iliyoambatana na uzinduzi wa kamati na shughuli za maandalizi ya Jubilee ya miaka mia moja ya seminari hiyo itakayofikia kilele mwaka 2025.


Mbunge huyo ameitikia mwaliko kutoka kwa Mhashamu baba Askofu Ludovick Minde wa Jimbo Katoliki la Moshi ambapo Misa takatifu iliadhimishwa na 
Mhashamu Askofu Mkuu Baba Isaac Amani wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha akishirikiana na Mhashamu Baba Askofu Ludovick Minde.



Katika uzinduzi huo, Mhashamu Baba Askofu aliipa mamlaka kamati kwa kuwaombea kuwabariki na kuwasha mshumaa wa uzinduzi.


Tukio hili lilihudhuriwa na Mapadri kutoka Parokia zote za Jimbo Katoliki  la Moshi, Watawa, Waseminaristi waliosoma katika shule hiyo kutoka sehemu mbalimbali nchini Tanzania na wageni waalikwa kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya mkoa wa Kilimanjaro.



Katika hafla hiyo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro Patrick Boisafi alialikwa hata hivyo alisoma katika Seminari hiyo. 



Katika uzinduzi huo, mbunge Ndakidemi alichangia shilingi Milioni moja.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI