Na Swalehe Magesa, Mwanza
MBUNGE wa Sengerema, Mhe. Hamis Hussein Mwagao Tabasam, amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kuwakumbuka viongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, pindi wanapomaliza shughuli hiyo.
Mhe. Tabasamu ameyasema hayo mapema leo, wakati mbio za Mwenge wa Uhuru, zikiwa wilayani Sengerema, ambapo pamoja na mambo mengine, umefungua miradi mbalimbali ya maendeleo.
"Viongozi hawa wa Mbio za Mwenge, Wana kazi kubwa mno, kuzunguka nchi nzima wakikagua miradi pamoja na kuibua ufisadi katika baadhi ya maeneo, ni ombi langu kwa Mhe. Rais kuwakumbuka vijana hawa, pindi wanapomaliza kazi hii kubwa kitaifa," alisema Mhe. Tabasamu.










0 Comments