Header Ads Widget

ZIPO FURSA 200 KWENYE CHIKICHI

 

Na MatukioDaimaAPP, Dar es salaam

Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania Tari kituo cha Kihinga Mkoani Kigoma Dr Filson Kagimbo amsema kuwa zipo fursa zaidi ya 200 kwenye  zao la chikichi ambapo amehimiza watanzania kuwekeza kwenye zao hilo ambalo ni mkombozi wa uchumi nchini. 


Kauli hiyo kaitoa jana kwenye maonyesho ya sabasaba ambapo alisema kuwa ili kuweza kumaliza upungufu wa mafuta nchini watanzania wanapaswa kulima zao hilo kwakuwa mafuta tunayotumia kutoka viwandani yanatokana na zao hilo. 


“Chikichi ni zao maarufu kwa uzalishaji wa mafuta aina mbili mawese na mise yanayotumika viwandani kwaajili ya kutengneneza sabuni, gundi, manukato na mishumaa  ni zao muhimu la kibiashara nizao pia kwaajili ya viwanda ndio maana tumekuja na mikakati kabambe ili kuhakikisha kuwa tunaboresha zao hilo na kuhimiza watanzania kuwekeza kwenye zao hilo kwa manufaa ya nchi”


“Zipo aina tatu  za chikichi ambazo ni dulla ambayo inalimwa kwa wingi lakini mafuta kidogo, wakati  Tenera inazalisha zaidi ya tani 5 kwa hekta  na Pisifela ndio maana tumekuja kuhamasisha watanzaniwa kuwekeza kwenye chikichi kwakutumia aina ya tenera ambayo inauzalishaji mkubwa zaidi” 


“Ukiangalia nchi yetu zao hili tumelima chini ya asilimia 0 na tunalo eneo kubwa linalofaa lakini tunalo eneo kubwa la nchi halijafikiwa na zao hili tunayonafasi kubwa kufanya uwekezaji huu muhimu kwa uchumi wan chi yetu ndio maana tunahamasisha watu kulima na kuleta mitambo ya kusindika na kusafisha kwakuwa linafaida kubwa mazao zaidi ya 200 unaweza kutoa kwenye chikichi”


MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI