Header Ads Widget

KESI YA WAKILI MADELEKA KUAMULIWA JULAI 29,2022

 



Teddy Kilanga_Arusha



Mahakama ya hakimu mkazi Arusha inatarajia kutoa maamuzi julai 29,2022  ya Maombi madogo ya jinai 1/2022 yaliyotolewa na  Peter Michael Madeleka  dhidi ya jamuhuri ya kumuondoa hatiani kutokana na hukumu ya kesi ya  ujuhumu uchumi namba  40/2020 



 Akipanga tarehe hiyo baada ya kusikiliza pande zote mbili,Hakimu mkazi wa mahakama hiyo,Herieth Mhenga alisema maombi hayo yatatolewa maamuzi julai 29 mwaka huu.




Kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 40/2020 iliyoamuliwa kwa njia ya makubaliano Kati ya mshtakiwa na Mwendesha Mashtaka wa Serikali nje ya mahakama na kupelekea Wakili Peter Madeleka kutoa kiasi cha  Tsh Mil 2 juu ya Makubaliano hayo na faini ya laki mbili kutoka kwa Mahakama. 




Kwa upande wake Wakili mwandamizi wa serikali Akisa Mhando alisema kwa mujibu wa vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo katika fedha ya uhujumu uchumi namba 40/2020 ya utakatishaji fedha iliyokuwa ikimkabili wakili Peter Madeleka inaonyesha kwamba yeye mwenyewe ndiye aliyeandika barua  ya kuomba pribageini.




"Barua hiyo aliiandika bila kushawishiwa akiwa na akili zake timamu hivyo naiomba mahakama isibadilishe kitu chochote kutokana na barua hiyo kuandika wakili Peter Madeleka lakini pia inaonyesha Peter Madeleka alileta risiti za malipo ya milioni mbili katika mahakama,"alisema Wakili Mhando.




Wakili Mhando alisema baada ya hapo pia hoja zilisomwa mahakamani na Peter Madeleka alikuwa na nafasi ya kupinga hoja hizo lakini hakupinga ikiwa hoja hiyo zilisomwa kwa lugha yake anayoielewa.




Akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama hiyo wakili Peter Madeleka alisema shauri hilo limesikilizwa katika mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mhenga kutokana na hoja zilizosikilizwa ambapo upande wa jamuhuri walipata nafasi ya kuzijibu.




"Hoja kubwa ya leo ni kulingana na yale makubaliano mwendesha mashtaka aliniamuru nikalipe pesa kama fidia kiasi cha sh. milioni mbili lakini kwa mujibu wa kanuni  ya pre bagain DPP haruhusiwi kupokea fedha kutoka kwa mtuhumiwa,"alisema Wakili Madeleka.





"Lakini nilimlipa DPP mnamo machi 30,2021 ikiwa ni takriba ni mwezi mzima kabla ya  hatujafanya makubaliano haya mahakamani na wakati huo nilikuwa gerezani hali ambayo nilikosa namna yeyote,"alisema.





Wakili Madeleka alisema lakini kwa kanuni za kisheria zinazosimamia pribageini DPP hapaswi kupokea fedha kutoka kwa mtuhumiwa hata kama kuna makubaliano na isitoshe kama fidia zitakuwa zikilipwa kwa serikali anayepaswa kuzipokea ni msajili wa hazina na hiyo ni kwa mujibu wa kanuni ya 21 ndogo ya 3A ya pribageini.




"Lakini hicho hakikufanyika  ikiwa kitendo hicho kinafanya kesi nzima pamoja na hukumu pamoja na adhabu ziweze kuwa ni batili kwa sababu hukumu yote ya mahakama na mwenendo wote wa kesi ili iweze kuwa halali lazima izingatie sheria,"alisema Madeleka.



Aidha Wakili Madeleka alisema wanasubiri maamuzi ya mahakama ataupokea maamuzi hayo yatakayotolewa na mahakama ya hakimu mkazi na hawatajali jinsi utakavyokuwa ikiwa kwa upande wao watachukua hatua ya kwenda mahakama za juu ikiwemo mahakama kuu na rufaa endapo ikibidi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS