Na Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam
Katika kuelekea mashindano ya mbio za Pikipiki yajulikanayo kama ‘EAST AFRICAN SUN VILLAGE ENDURO RACING 3’ yanatarajiwa kufanyika Julai 16 hadi 17 Wilayani Kibaha Mkoani Pwani maandilizi yamekamilika.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mwenyekiti wa Klabu ya waendesha pikipiki jijini Dar es salaam, Dar Riders Motor Sports Club (DRMSC),Ahmed Abdalla amesema kuwa mashindano hayo yatahusisha waendesha Pikipiki zaidi ya 40 kutoka ndani na nje ya nchi.
Amesema kuwa, mashindano hayo ambayo ni msimu wake wa tatu kwa mwaka huu pia yatahusisha waendesha pikipiki maalum kutoka nchi ya Kenya na Uganda.
Hata hivyo, amesema licha ya waendesha Pikipiki za Enduro lakini pia kutakua na madereva wa kawaida wa pikipiki maarufu kama bodaboda 20 ambapo yatatimua vumbi katika viunga vya mji wa Kibaha,Misugusugu.
Aidha ameongeza kuwa mashindano hayo yatashirikisha barabara mbalimbali ambazo tayari klabu ya DRMSC imeshaziandaa ikiwemo barabara za matope,mchanga,matuta na zenye kona kali ili kumpata dereva mahiri katika mashindano hayo.
Kwa upande wake, Katibu wa klabu hiyo ya waendesha pikipiki ya Dar es salaam, (DRMSC),Bazdawi Alsuary amewataka watanzania wajitokeze kwa wingi katika mchezo huo ili kushuhudia mbio hizo za pikipiki pamoja na madereva bodaboda ili wajifunze namna bora ya kuendesha pikipiki isiyo hatarishi.
No comments:
Post a Comment