Header Ads Widget

TEKNOLOJIA CHANGAMOTO KWA WASOMAJI WA VITABU

 


Na Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam 


Imeelezwa kuwa miongoni mwa changamoto zinazopelekea kupungua kwa wasomaji wa vitabu nchini Tanzania kwa miaka ya hivi karibuni ni kutokana na kuenea kwa Teknolojia ikiwemo simu na Television ikilinganishwa na mwaka 1970.


Akizungumza na Matukio Daima katika mahojiano maalum, Katibu wa Waandishi wa riwaya wenye dira (UWARIDI) Maundu Mwigizi amesema kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto hiyo lakini wamekua wakipambana kuhakikisha watanzania wanapenda kusoma vitabu mbalimbali ambavyo vimekua vikianzishwa.


"Zamani kulikua na wasomaji wengi wa vitabu kwa sababu hakukua na Teknolojia hivyo, watu wengi walikua wakipenda kusoma vitabu na kuwasimulia watoto hadithi, tofauti na sasa hivi lakini tunaendelea kupambana ili kurudisha kama ilivyokuwa zamani"amesema Maundu.


Aidha amesema wamejipanga kufanya mageuzi makubwa katika tasnia ya uwandishi wa riwaya, hivyo, wameiyomba Serikali kiwashika mkono katika kusimamia kazi zao ikiwemo kuchapisha vitabu na kupata Soko la uhakika.


Amesema kuwa, wamekua wakifanya matamasha mbalimbali ya uzinduzi wa vitabu ambapo wamekuwa wakishirikisha waandishi ambao hata sio wanachama wa Uwaridi na baadhi yao kuwatunukia ngao ya mtunzi.


"Tumeanzisha mfuko ambao unamuwezesha mwanachama kuweza kupata pesa za kuchapisha vitabu na baadae kuvipeleka sokoni, akiuza anarudisha pesa na mwengine Ili apate, lakini hii haitoshi tunaomba Serikali itusaidie"amesema Maundu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS