Header Ads Widget

KAMATI YA UTATU YAZAA MATUNDA, MADEREVA KULA SHAVU

 



Na Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam 


Baada ya Kamati ya utatu kufanya majadiliano baina ya viongozi wa vyama vya wafanyakazi, madereva na wamiliki wa vyombo vya usafirishaji, Serikali imeamuru wamiliki wa magari kuwalipa madereva wa magari yanayotoka Tanziania kuelekea nchini Kongo, shill 700,000 (Millage) na posho ya overstay baada ya siku 20 Dolla 10 za kimarekani kwa siku ambapo posho za return na kupakia na kushusha mzigo hazijafikiwa muafaka.


Kauli hiyo imetolewa na  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na watu wenye ulemavu Potras Katambi wakati akieleza hatua zilizochukuliwa na Serikali kuhusu hoja na malalamiko yaliyowasilishwa na wafanyakazi madereva na wamiliki wa vyombo vya usafirishaji nchini.



Amesema kuwa, hatua hiyo imekuja mara baada ya Serikali kusimamia kamati ya utatu ilioundwa kusimamia posho za safari kwa madereva baina ya viongozi wa vyama vya wafanyakazi, madereva na wamiliki wa vyombo vya usafirishaji nchini.

 

"Kuhusu posho za returns madereva walihitaji shill 350,000 na upande wa waajiri walifikia shill 300,000, na posho ya kushusha na kupakia mzigo madereva walihitaji dola 200 za kimarekani na waajiri walifikia dola 150 za kimarekani mpaka sasa hakuna muafaka uliofikiwa katika hili"amesema Naibu Waziri Katambi.



Ameongeza kuwa, viwango hivyo vya posho ni sehemu ya hali bora kwa wafanyakazi madereva ambavyo vitapaswa kuzingatia na waajiri katika mikataba ya ajira za madereva, ambapo Serikali itaendelea kufanya ukaguzi wa kazi ikiwa ni pamoja a kukagua mikataba hiyo kama imezingatia makubaliano hayo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI